Eustasi wa Antiokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya kwake.

Eustasi wa Antiokia (Side, Pamfilia, leo nchini Uturuki, karne ya 3 - Traianoupoli, leo nchi Ugiriki, karne ya 4) alikuwa askofu mkuu wa Antiokia wakati alipoushiriki Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325).

Kwa sababu ya kupinga sana Uario alipelekwa na kaisari Konstantino Mkuu uhamishoni huko Ulaya Kusini Mashariki na ndipo alipofariki dunia[1].

Mtu mwenye ujuzi mkubwa wa dini, anahesabiwa kati ya Mababu wa Kanisa ingawa kimetufikia kitabu chake kimoja tu[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kwenye 21 Februari.[3]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92835
  2. Comprehensive critical edition of Eustathius's oeuvre in Eustathius Antiochenus, Opera omnia. J.H. Declerck (ed.), Turnhout: Brepols, 2002 (Corpus Christianorum Series Graeca, 51), CDLXII+288 p., 155 x 245 mm, 2002 ISBN|978-2-503-40511-7
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.