Enriko wa Osso
Mandhari
Enriko wa Osso (jina kamili kwa Kihispania: Enrique de Ossó i Cervelló; Vinebre, Tarragona, Hispania, 16 Oktoba 1840 – Gilet, Valencia, Hispania, 27 Januari 1896) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki.
Pamoja na kuwa paroko, na kuwajibika hasa katika katekesi, alianzisha jumuia Kikosi cha Mt. Teresa wa Yesu kwa ajili ya malezi ya wasichana. Alipoondolewa, alikwenda kuishi kwa Ndugu Wadogo [1][2].
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 14 Oktoba 1979 na mtakatifu tarehe 16 Juni 1993.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Butler's Lives of the Saints Volume I, edited by Alban Butler and Paul Burns, pgs 201 and 202
- ↑ Saint Enric de Osso y Cervello. Saints SQPN (21 March 2016). Retrieved on 28 September 2016.
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |