Nenda kwa yaliyomo

Utitiri-mahameli mkubwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Dinothrombium tinctorium)
Utitiri-mahameli mkubwa
Utitiri-mahameli mkubwa
Utitiri-mahameli mkubwa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Nusungeli: Acari
Oda: Trombidiformes
Nusuoda: Prostigmata
Familia: Trombidiidae
Jenasi: Dinothrombium
Oudemans, 1910
Spishi: D. tinctorium
(Linnaeus, 1767)

Utitiri-mahameli mkubwa (Dinothrombium tinctorium) ni utitiri mkubwa wa familia Trombidiidae katika oda Trombidiformes ambaye ni baini ya spishi kubwa kabisa za matitiri (hadi mm 12).

Utitiri huyu ni mkubwa: mm 10-12, na ana rangi ya nyekundu kali. Ana miguu minane kama arakinida wote. Mwili umegawanywa katika gnathosoma na idiosoma kama matitiri wengine na pia umefunikwa kwa manyoya mengi kama mahameli.

Spishi hii hutokea maeneo ya jangwa na nusujangwa. Hatua zote za spishi hii huishi katika mchanga au ndani ya takataka za mimea na huonekana nadra. Wapevu hutokea baada ya mvua kubwa na kwa hivyo huitwa “rain bugs” (wadudu-mvua) kwa Kiingereza.

Mzunguko wa maisha

[hariri | hariri chanzo]

Jike anaweza kutaga mayai 100,000. Hatua ya kwanza inayotoka katika yai inaitwa pre-larva (hatua kabla ya lava), kisha kuna hatua moja ya lava, hatua tatu za tunutu (protonymph, deutonymph na tritonymph) na hatua ya mpevu. Pre-larva, protonymph na tritonymph hawana kinywa na miguu ni midogo sana au haiko. Lava ni vidusia wa nje juu ya arithropodi kama panzi, mbawakawa, vipepeo, buibui na buingamia. Deutonymph na wapevu ni mbuai wa arithropodi. Mbuawa wanaopendelewa na wapevu ni kumbikumbi.

Utetezi dhidi ya maadui

[hariri | hariri chanzo]

Rangi ya matitiri hao ni nyekundu kali kama onyo kwa maadui. Yaani wana ladha mbaya.