Nenda kwa yaliyomo

Christina Shusho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Christina Shusho
Jina la kuzaliwa Christina Shusho
Amezaliwa 24 Novemba 1978
Asili yake Mkoa wa Kigoma; ni Mbembe
Aina ya muziki Nyimbo za Injili

Kazi yake Mwimbaji wa Nyimbo za Injili
Ala Sauti
Aina ya sauti 3

Christina Shusho (alizaliwa Novemba mkoani Kigoma) ni mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania.

Maisha

Christina Shusho amezaliwa na kukua katika malezi mazuri ya dini ya Kikristo mkoani Kigoma.

Amesoma Shule ya Msingi na Sekondari hukohuko.

Aliolewa jijini Dar es Salaam na kujaliwa kupata watoto watatu.

Alianza kama mfanya usafi kanisani. Katika kazi yake ya usafishaji wa kanisa alifanikiwa kujiunga na kwaya, ndipo alipotumia kipaji chake cha kusifu. Miaka michache baadae aliamua kurekodi muziki wake mwenyewe.

Albamu yake ya kwanza ilikuwa ‘Kitu gani kinitenge na upendo wa Bwana’, ambayo ilimfanya ajiamini katika kuimba.

Albamu iliyofuata ni ‘Unikumbuke’ na ‘Nipe Macho’ ambayo imejulikana Afrika Mashariki.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Christina Shusho kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.