Christina Milian

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Christina Milian imeelekezwa hapa. Kwa albamu, tafadhali tembelea Christina Milian (albamu)

Christina Milian
Christina Milian 2008 akiwa katika sherehe za Billboard na Children Uniting Nations Oscar Party.
Christina Milian 2008 akiwa katika sherehe za Billboard na Children Uniting Nations Oscar Party.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Christine Flores
Amezaliwa 26 Septemba 1981 (1981-09-26) (umri 42)
Asili yake Jersey City,, Marekani
Aina ya muziki R&B
Kazi yake Mwimba
Mtunzi
Mwigizaji
Mnenguaji
Mtayarishaji
Ala Sauti
Miaka ya kazi 1998–present
Studio Def Soul, Island, MySpace
Tovuti ChristinaMilian.org

Christine Flores (amezaliwa 26 Septemba 1981) ni mtunzi, mwimbaji wa muziki wa pop na R&B, mtayarishaji, mnenguaji, na mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Christina Milian. Alizaliwa mjini Jersey City, New Jersey, halafu baadaye akahamia zake mjini Los Angeles. Akiwa na umri wa miaka ipatayo kumi na tatu, Milian akaanza kutamani kuwa mwigizaji.

Milian alipata kutoa albamu yake ya kwanza ya muziki iliyokwenda kwa jina lake mwenyewe, yaani Christina Milian, na wimbo maarufu kutoka katika albamu hiyo ni "AM to PM" na "When You Look at Me".

Nyimbo zote mbili zilipata kushika nafasi ya tatu katika chati bora za muziki wa Ufalme wa Muungano, lakini albamu yake haijapata kuuza nakala nyingi. Albamu ya pili ya Milian ni It's About Time, nayo haijafanikiwa kimauzo, lakini ilipokea Tuzo ya Grammy ikiwa kama albamu bora ya muziki wa R&B.

Wimbo maarufu kutoka katika albamu hiyo ni "Dip It Low", imekuwa nyimbo ya kwanza kwa umaarufu na kutunukiwa na Recording Industry Association of America kuwa kama wimbo bora kwa mauzo ya mtandaoni.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina la filamu Jina alilotumia Maelezo mengine
1996 Sister, Sister Lana Sehemu ya kwanza
1997 Smart Guy "TJ's Friend" Sehemu mbili
1998 A Bug's Life Sauti ya nyongeza
Movie Surfers Tina Flores Mfululizo wa kawaida
1999 Durango Kids Eleanor "Ellie" Bigelow
American Pie Band Geek Kauza sura
The Wood Msichana aliyekuwa anachezacheza Kauza sura
Clueless Megan Sehemu mbili
Get Real Tennisha Sehemu taru
Charmed Teri Lane Sehemu moja
The Steve Harvey Show "Young Lady in Hallway" Sehemu moja
The Amanda Show "Various roles" Sehemu moja
2003 Wannabes Host
Love Don't Cost a Thing Paris Morgan
2004 MTV Cribs Milian Sehemu moja
Torque Nina
2005 Man of the House Anne
Be Cool Linda Moon
2006 Pulse Isabell Fuentes
2007 Smallville Rachel Davenport Sehemu moja
Snowglobe Angela Moreno TV Movie
2008 Eight Days a Week Olivia Campbell Haijarushwa hewani
Need for Speed: Undercover Carmen Mendez
2009 The Ghosts of Girlfriends Past Bado inatayarishwa
Bring it On Cinco Lina Bado inatayarishwa

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]