Nenda kwa yaliyomo

Cannabidiol

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Cannabidiol

Cannabidiol (kwa Kiingereza pia: CBD oil) ni kiungo cha kemia kinachopatikana kiasilia katika bangi (Cannabis).

Kuna aina mbili za bangi: bangi na hemp. Hemp ndiyo chanzo kinachopendekezwa cha CBD.

Cannabidiol ilivumbuliwa mwaka 1940 na kusemekana kuwa ya maana kama dawa. CBD ni kati ya cannabidiods 113 zilizoko katika mmea wa mbangi na huwa asilimia arobaini katika ule mmea.

Shirika la Marekani la Food and Drug Administration (FDA) limepitisha Cannabidiol Epidiolex kwa matumizi katika kutibu ugonjwa wa kifafa kwa watoto.[1]

Cannabidiol yaweza kutumiwa mwilini kwa kuvuta moshi wa cannabis au kama kupulizwa kwa mdomo kwa presha. Yaweza pia kuchukuliwa moja kwa moja kutokana na mafuta ya CBD ambayo haina THC. THC ndiyo kiungo ambacho kinalewesha katika bangi. CBD haileweshi kama THC ingawa kuna wanaouza CBD ikiwa na THC bila kuwaambia wanaonunua.

Madhara ya Cannabidiol ni kama vile: uchovu na kulala sana, kukosa hamu ya chakula, kuhara pamoja na kujisikia mwili umenyongonyea[2].

Historia ya Cannabidiol

Cannabidiol kwanza iliweza kudondolewa mwaka 1940 na wanasayansi wawili, Adams na Todd. Kwa wakati ule walidhania kwamba kiungo hiki kuwa hakina nguvu zozote za kibaolojia. Lakini mwaka 1963, wanasayansi wawili tena, Mecholaum na Shvo waliweza kuchunguza kwa kina kuhusu muundo wa kikemia wa cannabidiol.

Matumizi ya Cannabidiol

Cannabidiol inatumika kwa kupunguza maumivu mwilini japo matumizi yake hayajakubaliwa na nchi nyingi. Katika nchi ambazo matumizi yake yamekubaliwa, hutumika kwa njia hizi.

CBD hutolewa katika mmea wa hemp haswa kutokana na nguvu yake kubwa ambayo ni muhimu kwa matumizi ya matibabu. Wapo wanaotaja faida kadhaa za CBD:

  • Uondoaji wa maumivu sugu
  • Inayo mali kadhaa ya neuroprotective
  • Utoaji wa maumivu sugu Inayo mali kadhaa ya neuroprotective Inaweza kupunguza athari za chunusi
  • Inayo mali ya kukandamiza
  • Inaweza kusaidia katika matibabu ya ugonjwa wa kisukari cha aina 1
  • Inatumika katika matibabu ya magonjwa ya moyo

Kifafa

Maandishi ya kimatibabu yaliyochapishwa mwaka 2017 na 2018 yanaonyesha utafiti umefanywa kuonyesha kwamba CBD oil inaweza kutibu kifafa kwa watoto. FDA ilipitisha Epidiolex kwa kutibu Lennox-Gastaut na Dravet Syndromes za kifafa.

Multiple sclerosis pain

Nchini Kanada na Sweden, dawa ya Nabiximols inayotokana na cannabidiol imepitishwa kwa kupunguza maumivu ya multiple sclerosis. Kwa hii dawa, CBD na THC huchanganyishwa kwa uwiano wa moja kwa moja.

Ugonjwa wa Parkinson

Cannabidiol hutumika katika kupunguza wasiwasi (anxiety) kwa watu walio na ugonjwa wa Parkinson

Maamkizi ya CBD na serikali za nchi

Chakula na vinywaji vyenye mafuta ya CBD vilianza kuingia nchini Marekani mwaka wa 2017. Hata hivyo kuna wale wanaouza mafuta hayo bila ya wanunuzi kujua kuwa chakula walichokinunua kina cannabidiol na wamepata barua za onyo kutoka shirika la Food and Drug Administration (FDA). Pia kuna wanaodondoa mafuta ya CBD kutoka kwa mbangi kwa njia isiyokubalika.

FDA imesema kuwa unapotafuta mafuta ya CBD, uangazie mambo haya:

Njia ya kukuza mmea

Kuna wale wanaotumia kemia kukuza mimea ya mbangi ambayo hutoa mafuta ya CBD. Hili halifai kwa sababu huenda ukadhuru afya yako ukitumia cannabidiol iliyokuzwa kwa njia hii.

Njia ya kudondoa cannabidiol kutoka mmea

Muundo wa kudondoa cannabidiol kutokana na mmea una maana sana. Kampuni nyingi zatumia njia hafifu kwa kutumia kemia zenye madhara kama vile propane, pentane na butane ambazo zinaweza kuwaka, tena kuacha kemikali mwilini.

Viungo vya mafuta ya CBD

Huenda mafuta ya CBD unayotumia ikawekwa viungo vingine visivyo sawa na mwili wako. Yafaa basi uangalie viungo hivyo kwa makini usije ukadhurika. Loyal THC inasema kuwa yafaa pia cannabidiol ipitishwe katika maabara ili unapotumia, uwe unajua fika ni nini kilichomo katika mafuta ya CBD oil unayotumia.

Marejeo

  1. James Rivers (2020-04-13). "FDA Regulation About CBD And Cannabis Products: Epidiolex". CBDSold | CBD Products News | CBD Oil News (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-03. Iliwekwa mnamo 2020-07-02.
  2. In many communities, cannabis is perceived as a low-risk drug, leading to political lobbying to decriminalise its use. Acute and chronic cannabis use has been shown to be harmful to several aspects of psychological and physical health, such as mood states, psychiatric outcomes, neurocognition, driving and general health. Furthermore, cannabis is highly addictive, and the adverse effects of withdrawal can lead to regular use. These in turn have adverse implications for public safety and health expenditure. Although the cannabinoid cannabidiol (CBD) has been shown to have positive health outcomes with its antioxidant, anticonvulsant, anti-inflammatory and neuroprotective properties, high-potency cannabis is particularly damaging due to its high tetrahydrocannabinol (THC), low CDB concentration. It is this high-potency substance that is readily available recreationally. While pharmaceutical initiatives continue to investigate the medical benefits of CDB, “medicinal cannabis” still contains damaging levels of THC. Altogether, we argue there is insufficient evidence to support the safety of cannabis and its subsequent legalisation for recreational use. Furthermore, its use for medicinal purposes should be done with care. We argue that the public conversation for the legalisation of cannabis must include scientific evidence for its adverse effects. . http://www.eurekaselect.com/154161/article

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cannabidiol kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.