Nenda kwa yaliyomo

Bibi Titi Mohammed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bibi Titi Mohamed)
Bibi titi mohamed

Amezaliwa 1926
Dar es Salaam
Amekufa Novemba 5,2000
Nchi Tanzania
Chama cha kisiasa TANU
Waliosimama wa pili kushoto ni Ali Msham (Mwenyekiti wa Tawi la Magomeni Mapipa), wa nne ni Bi. Khadija biti Jaffar, wa tano Bi. Mtendwa biti Iddi Sudi, wa sita biti Feruzi, wa saba Mama Tindwa. Waliokaa wa kwanza ni Mzee Mwinjuma Mwinyikambi, wa tatu ni Bi. Titi Mohamed na pembeni ni mwanae.

Bibi Titi Mohammed (1926 - 5 Novemba 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza mzalendo kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.[1]

Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.

Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlaani.

Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye maandishi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".

Tarehe 5 Novemba 2000 Mohammed alifariki kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.[2][3]

Moja kati ya mabarabara makubwa ya jijini Dar es Salaam limepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.

  1. Deutsche Welle (www.dw.com). "Bibi Titi Mohamed: "Mama wa Taifa" Tanzania | DW | 03.03.2020". DW.COM. Iliwekwa mnamo 2020-08-21.
  2. Makala kuhusu kufa kwa Mpigania Uhuru Bi. Titi Mohammed
  3. https://www.bbc.com/swahili/habari-45967916

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bibi Titi Mohammed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.