Benedikto, Yohane na wenzao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kifodini chao.

Benedikto, Yohane na wenzao Mathayo na Isaka (waliuawa Kazimierz, leo nchini Polandi, 12 Novemba 1003) walikuwa wamonaki wa urekebisho wa Wabenedikto wa Camaldoli.

Mwaka 1001 Padri Benedikto wa Benevento na Yohane wa Cervia walitumwa na Romwaldo kutoka Italia wakafanye umisionari huko Polandi walipopata mapema kifodini pamoja na manovisi 2 wazawa na mtumishi Kristiano. Ndio wafiadini wa kwanza wa Polandi.

Tangu kale Benedikto na wenzake wanaheshimiwa kama watakatifu. Papa Julius II alithibitisha heshima hiyo mwaka 1508[1].

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Novemba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91865
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.