Nenda kwa yaliyomo

Romualdo Abati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Guercino, San Romualdo, Ravenna.

Mtakatifu Romualdo (Ravenna, Emilia-Romagna, 951 / 953 - karibu na Fabriano, Marche, 19 Juni 1027) alikuwa abati nchini Italia na mwanzilishi wa urekebisho wa Wabenedikto Wakamaldoli.

Anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki kuanzia miaka 5 baada ya kufa, na hasa tangu mwaka 1595.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 19 Juni[1].

Maisha yake yamesimuliwa na mfuasi wake Petro Damiani katika kitabu alichokiandika miaka 15 hivi baada ya kifo chake (1042)[2].

Kitabu rasmi cha watakatifu wa Kanisa la Roma (Martirologium Romanum) kinamkumbuka hivi: "Mtakatifu Romualdo, mkaapweke na baba wa wamonaki Wakamaldoli, ambaye, akiwa na asili ya Ravenna, na kutamani kushika maisha na nidhamu ya wakaapweke, alizunguka Italia miaka mingi, akijenga monasteri ndogo na kuhimiza kokote wamonaki wafuate maisha ya Kiinjili, mpaka alipomaliza vizuri juhudi zake katika monasteri ya Val di Castro mkoani Marche". [3].

Sala yake

[hariri | hariri chanzo]

Yesu mpenzi, amani ya moyo wangu, hamu isiyosemeka, utamu na unono wa malaika na wa watakatifu!

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum
  2. Sehemu kuhusu kifo chake imetafsiriwa kwa Kiswahili katika Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 195-196
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/27750

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 210-211
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 176-177

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.