Barlaam wa Antiokia
Mandhari
Barlaam wa Antiokia (alifariki Antiokia, leo nchini Uturuki, 303 hivi) alikuwa mkulima asiyejua kusoma wala kuandika aliyeuawa katika dhuluma wa kaisari Dioklesyano dhidi ya Ukristo[1][2] Akiimarishwa na hekima ya Kristo, alipopewa makaa ya moto na ubani ili kutoa sadaka kwa miungu, alivishika mkononi kwa imani isiyoshindika hadi ukatili wa dhalimu ulipomuua.[3].
Basili Mkuu, Yohane Krisostomo na Severo wa Antiokia walihubiri juu yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Novemba[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |