Austremoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake huko Issoire.

Austremoni (alifariki Clermont Ferrand, Akwitania, leo nchini Ufaransa, 286 hivi) alikuwa askofu kutoka Roma ambaye aliinjilisha mji wa Clermont Ferrand na Auvergne kwa jumla[1][2][3].

Kadiri ya wanahistoria Wakristo[4]. chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Novemba[5].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/93120
  2. "Historia Francorum, i.30". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-14. Iliwekwa mnamo 2020-10-30. 
  3. Goyau, Georges. "Diocese of Clermont." The Catholic Encyclopedia Vol. 4. New York: Robert Appleton Company, 1908. 12 April 2019
  4. The Vetus Martyrologium Romanum (1961) under Die 18 Decembris: Quintodecimo Kalendas Januarii: "Turonis, in Gallia, Sancti Gatiani Episcopi, qui, a Sancto Fabiano Papa primus ejusdem civitatis Episcopus ordinatus est, et multis clarus miracolis obdormivit in Domino".
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.