Atenodoro wa Kaisarea
Atenodoro wa Kaisarea (Kaisarea Mpya, 215 hivi – Kaisarea Mpya, Ponto, leo nchini Uturuki, 270 hivi) alikuwa askofu wa karne ya 3.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Novemba[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Atenodoro alikuwa mdogo wa Gregori Mtendamiujiza. Familia yao ilikuwa haijaingia dini hiyo, ambayo yeye alikuja kuifahamu akiwa na umri wa miaka 12, baada ya kufiwa baba yake.
Pamoja na kaka yake, Atenodori alikuwa ametumwa Beirut (leo nchini Lebanon) kwa ajili ya masomo ya sheria; kutoka huko walisafiri hadi Kaisarea ya Palestina. Huko walisikia habari za msomi maarufu Origen, mkuu wa Chuo cha Katekesi cha Aleksandria, aliyekuwa anaishi huko. Udadisi uliwafanya wakamsikilize na kuongea naye; ndipo walipovutiwa sana, kiasi cha kusahau kabisa Beirut na sheria.
Umaarufu alioupata kwa kushirikisha ujuzi wake wa Biblia ulifanya apewe daraja takatifu hiyo akiwa bado kijana (260 hivi) [2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/76380
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |