Nenda kwa yaliyomo

Moses Kulola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Askofu moses kulola)

Moses Kulola (Juni 1928 - Agosti 2013) alikuwa kiongozi wa Kikristo nchini Tanzania na tangu mwaka 1991 askofu wa EAGT (Evangelistic Assemblies of God Tanzania).[1]

Pia historia hii inapatikana katika Blog ya Tanzania Gospel Network Ilihifadhiwa 17 Mei 2013 kwenye Wayback Machine.

Moses Kulola alizaliwa mwezi Juni 1928 katika familia ya watoto kumi, watano kati yao wakiwa bado hai mwaka 2013.

Alisajiliwa kwanza katika shule ya misheni iitwayo Ligsha Sukuma mwaka 1939, halafu alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949.

Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.

Alimwoa Elizabeth na kuzaliana naye watoto 10 ambapo saba walikuwa bado hai alipofariki.

Alianza kazi za umisionari mwaka 1950 mara tu baada ya kubatizwa, ijapokuwa aliitwa mwaka 1949.

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huohuo akihubiri Injili katika miji na vijiji.

Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifikia mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake, mwili na nafsi.

Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha teolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Alijiendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti katika mataifa mbalimbali.

Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa Mpentekoste mnamo 1961-1962.

Alifanya kazi katika kanisa la TAG tangu mwaka 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzisha kanisa la Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambalo lilifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia, Malawi na kwa jumla lina makanisa yapatayo 4000 yakiwemo makubwa na madogo.

Askofu Msaidizi wake alikuwa Mwaisabila.

Kumefanyika mgawanyiko wa majimbo 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi, kila kanda na jimbo likiwa na mwangalizi wake.

Alifariki mwano Agosti 2013 na kuzikwa mjini Mwanza katika kanisa linalogombaniwa na TAG na EAGT.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. tanzaniagospel.blogspot.com