Bundi (Strigidae)
Bundi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 3 (pamoja na 1 ya Striginae): |
Bundi (pia mabundi) ni ndege mbuai wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Ukurasa huu unahusu familia Strigidae. Spishi hizi zinaainishwa katika nusufamilia Asioninae na jenasi moja ya nusufamilia Striginae.
Bundi hawa wana kichwa kikubwa chenye umbo la mviringo, mkia mfupi na rangi ya kamafleji. Kwa kawaida jike ni mkubwa kuliko dume. Mabawa yao ni marefu na mapana. Hula ndege na wanyama wadogo, wanyama wagugunaji hasa, lakini watambaachi na wadudu wakubwa pia. Jike huyataga mayai 2-7 katika tundu la mti au tago lililoachwa na ndege mwingine, pengine katika sanduku la kutagia.
Bundi wengi huwinda usiku na hupumzika mchana. Wanamlenga mbuawa wao kwa msaada ya masikio yao. Manyoya ya uso yapeleka mawimbisauti kwa vipenyo vya masikio ambavyo kimoja kipo juu kidogo kuliko kingine. Hivyo wanaweza kumkamata mbuawa bila kumwona. Mbuawa hawezi kumsikia bundi akija, kwa sababu mabawa ya bundi hayafanyi sauti yo yote kwa kuwa kingo ya mbele ya manyoya ya mabawa imekerezekakerezeka na ile ya nyuma ina matamvua. Hii inapunguza vurugu ya hewa na kwa hivyo uvumi.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Asio abyssinicus, Bundi Masikio-marefu (Abyssinian owl)
- Asio capensis, Bundi-maji (Marsh owl)
- Asio flammeus, Bundi Masikio-mafupi (Short-eared owl)
- Asio madagascariensis, Bundi wa Madagaska (Madagascan owl)
- Asio otus, Bundi wa Ulaya (Long-eared owl)
- Strix aluco, Bundi Hudhurungi (Tawny owl)
- Strix hadorami, Bundi-jangwa (Desert owl)
- Strix woodfordii, Bundi-misitu (African wood owl)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Asio stygius (Stygian owl)
- Nesasio solomonensis (Fearful owl)
- Pseudoscops clamator (Striped owl)
- Pseudoscops grammicus (Jamaican owl)
- Strix albitarsis (Rufous-banded owl)
- Strix butleri (Omani owl)
- Strix chacoensis (Chaco owl)
- Strix davidi (Père David's owl)
- Strix fulvescens (Fulvous owl)
- Strix huhula (Black-banded owl)
- Strix hylophila (Rusty-barred owl)
- Strix leptogrammica (Brown wood owl)
- Strix nebulosa (Great grey owl)
- Strix nigrolineata (Black-and-white owl)
- Strix nivicolum (Himalayan owl)
- Strix occidentalis (Spotted owl)
- Strix ocellata (Mottled wood owl)
- Strix rufipes (Rufous-legged owl)
- Strix sartorii (Cinereous owl)
- Strix seloputo (Spotted wood owl)
- Strix uralensis (Ural owl)
- Strix varia (Barred owl)
- Strix virgata (Mottled owl)
Spishi ya kabla ya historia
[hariri | hariri chanzo]- Asio brevipes (Mwisho wa Pliocene ya Hagerman, MMA)
- Asio priscus (Mwisho wa Pliocene ya Kisiwa cha Santa Rosa, MMA)
- Strix brea (mwisho wa Pleistocene ya Amerika ya Kaskazini)
- Strix dakota (mwanzo wa Miocene ya South Dakota, MMA) – labda haistahili kuwa katika jenasi Strix
- Strix edwardsi (kati ya Miocene ya Grive-Saint-Alban, Ufaransa) – labda yastahili kuwa katika jenasi Ninox
- Strix ignota (kati ya Miocene ya Sansan, Ufaransa) – labda haistahili kuwa katika jenasi Strix
- Strix intermedia (mwanzo – kati ya Pleistocene ya Ulaya ya Kati) – labda ni spishi ndogo ya S. Aluco ambayo imekwisha sasa
- Strix wintershofensis (mwanzo – kati ya Miocene ya Wintershof, Ujerumani wa Magharibi) – labda yastahili kuwa katika jenasi Ninox
- Strix sp. (mwisho wa Miocene ya Nebraska, MMA)
- Strix sp. (mwisho wa Pliocene ya Rębielice Królewski, Poland)
- Strix sp. (mwisho wa Pleistocene ya Ladds, MMA)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Bundi-maji
-
Bundi masikio-mafupi
-
Bundi wa Madagaska
-
Bundi wa Ulaya
-
Bundi hudhurungi
-
Bundi-jangwa
-
Bundi-misitu
-
Stygian owl
-
Black-banded owl
-
Black-and-white owl
-
Mottled owl
-
Striped owl
-
Jamaican owl
-
Fulvous owl
-
Rusty-barred owl
-
Brown wood owl
-
Great grey owl
-
Spotted owl
-
Mottled wood owl
-
Rufous-legged owl
-
Spotted wood owl
-
Ural owl
-
Barred owl