Nenda kwa yaliyomo

Arseni Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani kwenye mlima Athos, karne ya 14.

Arseni Mkuu, au Arseni shemasi au Arseni wa Scetis au Arseni Mrumi (Roma, 350/354 - Troe, Misri 445) alikuwa msomi na tajiri wa Roma ambaye, baada ya kulea watoto wa kaisari Theodosius I kwa miaka 11, akiwa shemasi, alihamia jangwani huko Misri ili aishi kama mkaapweke kwa miaka 55.

Ni kati ya mababu wa jangwani walioacha athari kubwa zaidi katika maisha ya Kiroho ndani ya Kanisa[1], ndiyo sababu aliitwa "mkuu".

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kwa kawaida tarehe 8 Mei[2], isipokuwa na Wakhufi[3][4].

Maandishi

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya vitabu alivyoandika, viwili vipo hadi leo: mwongozo wa maisha ya kimonaki (διδασκαλία και παραινεσις = Fundisho na Angalisho), na ufafanuzi wa Injili ya Luka (εις τον πειρασθεν νομικος = Kuhusu Kishawishi cha Sheria).

Mbali ya hivyo, misemo yake mingi inapatikana katika Apophthegmata Patrum.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. de Sales, St. Francis (2013). The Complete Introduction to the Devout Life. Brewster, Massachusetts: Paraclete Press. uk. 325. ISBN 1612612350.
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. Martyrologium Romanum (2001), http://www.diocesisdecanarias.es/downloads/santosmartirologioenerojunio.pdf Archived 19 Mei 2017 at the Wayback Machine..
  4. Ὁ Ὅσιος Ἀρσένιος ὁ Μέγας. 8 Μαΐου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints, 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.