Apolinari wa Valence
Mandhari
Apolinari wa Valence (Vienne, Ufaransa, 453 hivi – 520 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 490 hivi.
Baba yake, Esiki wa Vienne, alikuwa seneta, halafu askofu wa Vienne, kabla ya mtoto wake mwingine, Avito wa Vienne.
Apolinari alikuwa mwenye ari sana kwa ajili ya haki na maadili akafaulu kurudisha mamlaka na heshima ya Ukristo katika jimbo lake baada ya hilo kubaki muda mrefu bila askofu[1].
Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Oktoba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |