Amatori wa Auxerre
Mandhari
Amatori wa Auxerre (kwa Kifaransa: Amadour au Amatre; alifariki Auxerre, leo nchini Ufaransa, 1 Mei 418) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 388 hadi kifo chake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 1 Mei[1][2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Amatori alisoma teolojia chini ya Valeriani wa Auxerre, lakini wazazi walimshinikiza kuoa. Hata hivyo alikubaliana na mke wake kuishi kama kaka na dada.
Baadaye mkewe alijiunga na umonaki, naye alijiunga na kleri[3] na hatimaye akawa askofu kwa miaka 30 akijitahidi kung'oa ushirikina na kueneza heshima kwa wafiadini[4].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Ὁ Ἅγιος Ἀγαπητὸς Ἐπίσκοπος Ὡξέρρης. 1 Μαΐου. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.
- ↑ Butler, Alban. “Saint Amator, Bishop of Auxerre, Confessor”. Lives of the Fathers, Martyrs, and Principal Saints, 1866. CatholicSaints.Info. 4 May 2013
- ↑ Monks of Ramsgate. “Amator”. Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 30 May 2012
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saint of the Day, May 1: Amator Archived 21 Desemba 2010 at the Wayback Machine.
- Cathédrale Saint-Étienne (Image of St. Amadour)
- Procesión de San Amador, patrón de Martos (Jaén), el 5 de Mayo de 2006
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |