Nzi mweupe
Nzi mweupe | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nzi mweupe wa kiazi kitamu (Bemisia tabaci)
| ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||||
Nusufamilia 3:
|
Nzi weupe ni wadudu wadogo wa familia Aleyrodidae katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wadudu hawa wanaweza kuwa wasumbufu kama vidukari, hususa wakiwa tele, kwa sababu wanafyunza utomvu pia na kuvu nyeusi inakua juu ya mana wanayochoza na inayoanguka kwenye majani. Kuvu hii inazuia majani yasifanye usanidimwanga na mmea unanywea. Lakini hasara kubwa zaidi inayosababishwa na nzi weupe ni uwezo wao wa kusambaza magonjwa ya virusi za mimea. Kwa mfano, nzi mweupe wa kiazi kitamu anaweza kusambaza zaidi ya spishi kumi za virusi: virusi ya mosaiki ya mhogo ya Afrika (ACMV), virusi ya mosaiki ya dhahabu ya mharagwe, virusi ya mkunjo njano ya mnyanya (TYLCV) n.k. Nzi weupe wana adui wao kama wadudu-kibibi, wadudu mabawa-vena, wadudu-maua, nyigu wa kidusia n.k. Pia kuna kuvu viuawadudu (entomopathogenic fungi) inayoambukiza lava wa nzi weupe, kama Beauveria bassiana, Isaria fumosorosea na Metarhizium anisopliae.
Nzi weupe ni wadudu wadogo. Wapevu wa takriban spishi zote wana urefu wa mm 1-3, lakini spishi chache zinaweza kufika mm 5. Kiwiliwili cha nzi weupe kimerefuka kidogo na kinabeba mabawa manne ya ukubwa sawa ambayo yamepakiwa nta. Nta hii inawapatia rangi ya nyeupe. Vipande vya mdomo vimeungana katika mrija utumikao ili kufyunza utomvu. Hatua zote za nzi weupe (mayai, lava, wapevu) hupatikana kwa upande wa chini wa majani kwa kawaida.
Spishi zilizochaguliwa
[hariri | hariri chanzo]- Aleurocanthus spiniferus, Nzi Kijivu wa Mchungwa (Orange spiny whitefly)
- Aleurocanthus woglumi, Nzi Mweusi wa Mchungwa (Citrus blackfly)
- Aleurodicus dispersus, Nzi Mweupe wa Miti (Spiralling whitefly)
- Aleurothrixus floccosus, Nzi Mweupe Sufu (Wooly whitefly)
- Bemisia tabaci, Nzi Mweupe wa Kiazi Kitamu (Sweet potato whitefly)
- Trialeurodes ricini, Nzi Mweupe wa Mbarika (Castor withefly)
- Trialeurodes vaporariorum, Nzi Mweupe wa Mboga (Greenhouse whitefly)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Nzi mweusi wa mchungwa
-
Lava wa nzi mweusi wa mchungwa
-
Nzi mweupe wa kiazi kitamu
-
Lava wa nzi mweupe wa kiazi kitamu
-
Nzi mweupe wa mboga
-
Lava wa nzi mweupe wa mboga
-
Nyigu wa kidusia, Eretmocerus hayati
-
Lava wa nzi mweupe wa kiazi kitamu aliyeuawa na lava wa nyigu wa kidusia
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nzi mweupe kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |