Usanisinuru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Usanidimwanga)
Kila jani kina kiwanda cha kikemia ndani yake.

Usanisinuru (pia usanidimwanga, ing. photosynthesis) ni mchakato wa kibiolojia na kikemia ambako mimea ya kijani inageuza nguvu ya nuru ya jua kuwa nishati ya kikemia. Inatengeneza kabohidrati ikitumia nguvu ya nuru ya jua na dioksidi kabonia ya hewani pamoja na maji.

Nje ya mimea kuna pia aina kadhaa za bakteria na hasa mwani zinazofanya usanisinuru.

Fomula yake ni

6 CO2 + 12 H2O + nuru → C6H12O6 + 6 O2 + 6 H2O
dioksidi kabonia + maji + nishati nuru → glukosi + oksijeni + maji

Usanisinuru ni msingi wa maisha yote duniani. Unajenga mada ogania ambayo ni chanzo cha lishe katika mtando chakula kwa karibu viumbehai vingine vyote kwa njia moja au nyingine. Kwa njia hii ni chanzo cha mtando chakula wa uhai wote.

Mchakato wa usanisinuru[hariri | hariri chanzo]

Picha ya kiwiti (chloroplast)

Usanisinuru unaanza kwenye sehemu za kijani za majani. Rangi ya kijani inatokana na punje ndogo sana za kiwiti ndani ya majani. Wakati nuru ya jua inafikia kiwiti inasababisha kemikali ndani yake kuvunja molekuli za maji. Molekuli ya maji ikivunjwa inatoa oksijeni, hidrojeni na nishati. Protini ndani ya seli inatumia dutu hizi pamoja na dioksidi kabinia ya hewani kujenga glukosi na ATP ambayo ni molekuli ya fosifati inayotunza nishati nyingi ndani ya muungo kemia wake.

Katika mchakato huu oksijeni inaachishwa na hivyo usanisinuru ni pia chanzo cha oksijeni katika angahewa ya dunia jinsi ilivyo.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usanisinuru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.