Mtando chakula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mfano wa mtando chakula katika bahari ya aktiki

Mtando chakula ni neno la kutaja uhusiano kati ya viumbehai mbalimbali katika mazingira fulani.

Mfano chepesi ni: panya anayekula nafaka analiwa na nyoka; nyoka analiwa na tai; tai kwa kawaida hana adui anayemshinda lakini akifa mwili wake analiwa na sisimizi na labda tena panya mwingine. Kama mwili waka unaoza bila kuliwa unageukia kuwa tena minerali zitakazolisha mimea ambayo ni tena chakula cha panya.

Hali halisi uhusiano katika mitando ya chakula si chepesi hivi kwa sababu kuna spishi nyingi zaidi zinazoshiriki mle.

Njia nyingine ya kuitazama ni namna gani nishati inapitishwa kutoka spishi moja kwenda kwa nyingine.

Karibu kila mtando chakula huanzishwa kwa nguvu ya nuru ya jua; nishati hii inapokelewa na mimea kwa njia usanisinuru na kutumiwa kwa kujenga mwili wa mmea mwenyewe. Mimea hii huliwa na wanyama wala majani ambao tena huliwa na wanyama wengine wala nyama. Miili ya wanyama hao wakifa inaoza tena pamoja na sehemu za mimea ambayo hayaliwi na yote inarudi kuwa sehemu ya udongo.

Picha katika makala hii inaonyesha sehemu ya mtando chakula katika bahari ya Aktiki:

  1. . chanzo ni nuru ya jua inayolisha
  2. . planktoni mimea (phytoplanktoni) inayolisha
  3. . planktoni wanyama (zooplanktoni) inayolisha
  4. . samaki wengi wadogo lakini pia aina mbalimbali za samaki wakubwa hadi nyangumi.
  5. . Samaki huliwa na wanyama wengine kama ndege za bahari, sili, papa na wakati mwingine hata dubu aktiki.
  6. . Sili ni chakula cha papa na dubu aktiki.