Nenda kwa yaliyomo

Musoma (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wilaya ya Musoma mjini)


Musoma
Musoma is located in Tanzania
Musoma
Musoma

Mahali pa mji wa Musoma katika Tanzania

Majiranukta: 1°29′24″S 33°48′0″E / 1.49000°S 33.80000°E / -1.49000; 33.80000
Nchi Tanzania
Mkoa Mara
Wilaya Musoma Mjini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 164,172
Msimbo wa posta 31101 - 31113  

Musoma ni mji wa Tanzania uliopo kwenye mwambao wa mashariki wa Ziwa Viktoria. Musoma imepata halmashauri na hadhi ya manisipaa. Manispaa hiyo inapakana na Wilaya ya Musoma Vijijini.

Ni makao makuu ya Mkoa wa Mara.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa mji huo ilihesabiwa kuwa 108,242 [1] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 164,172 [2].

Tembo beach.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ukoloni eneo la Musoma lilikuwa nchi ya Wakabwa, kundi la Wajaluo waliowahi kuhamia hapa.[3]

Wajerumani wa kwanza walifika mnamo mwaka 1910: walikuwa wamisionari, kwa majina Dominik na Paulo, waliojenga makazi na shule karibu na makao ya Mtemi Nyabange[4].

Wakafuatwa na afisa wa kwanza Mjerumani aliyeitwa na wenyeji "Bwana Sirusi" mwenye kazi ya afisa forodha. Huyu Sirusi alihamia mahali pa Musoma ya leo kwa sababu huko kina cha maji ufukoni kilifaa zaidi kwa meli kufika[5]. Hivyo Musoma ilianzishwa kama bandari na baadaye makao ya ofisa mdogo wa Mkoa wa kikoloni wa Mwanza.

Baada ya kuondolewa kwa Wajerumani, Waingereza waliingia. Katika eneo la kudhaminiwa la Tanganyika Musoma ilikuwa makao makuu ya wilaya (district) ikaingia vile katika Tanzania huru.

Mwalimu Julius Nyerere alisoma shule Musoma kuanzia mwaka 1934 na tarehe 21 Januari 1953 alirudi huko kufunga ndoa na Maria Waningu Gabriel Magige katika Kanisa Katoliki la Musoma Mwisenge [6].

  1. "Matokeo ya sensa ya 2002 kwa mkoa wa Mara". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2003-12-18. Iliwekwa mnamo 2003-12-18.
  2. https://www.nbs.go.tz
  3. Siso - Shetler, uk. 75
  4. Kutokana na maelezo katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani Nyabange iliyoitwa "Njawangi" (jer. "j"=y) ilikuwapo takriban kilomita 10 upande wa mashariki wa Musoma kwenye mwambao wa hori ya ziwa, angalia makala "Muansa" na "Njawangi" katika kamusi hii
  5. Siso - Shetler, uk. 79
  6. Thomas Molony, Nyerere: The Early Years , Boydell & Brewer Ltd, 2014 , uk. 189

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Kata za Wilaya ya Musoma Mjini - Mkoa wa Mara - Tanzania

Buhare | Bweri | Iringo | Kamunyonge | Kigera | Kitaji | Kwangwa | Makoko | Mshikamano | Mukendo | Mwigobero | Mwisenge | Nyakato | Nyamatare | Nyasho | Rwamlimi


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Musoma (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.