Wakabwa
Wakabwa ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mara. Lugha yao ni Kikabwa.wanapatikana katika vijiji vya Bukabwa na Mmazami idadi yao ni karibu 4000.mila na desturi zao zinaelekeana na koo nyingine za kikurya.kwani wao nao wana mila na taratibu kama koo nyingine za kikurya lugha na wanachokiongea hakina tofauti na yanayojiita makabila ya kikurya japokuwa ni koo tu.matamshi yao yanaelekena na Wasweta ambao hupatikana kwa wingi wilaya ya Tarime kandokando ya ziwa victoria jirani na ABHASIMBETE(WASIMBITI).Shughuli zao kubwa ni ukulima wa uwele mtama mhogo na ufugaji wa wanyama mbalimbali wafugwao kama ng'ombe,mbuzi,na kondoo.pia ni watu wanaomini sana kuhusu uchawi ndoo maana hata vijiji vyao vimeshindwa kufanya maendeleo ya haraka kwa kuhofia kulogwa.Wengi wao wanapatikana katika kijiji cha magana na kirumi.Wanatahiri wananume na kukeketa wasichana ingawa mila hii ya kukeketa wasichana inaelekea kuisha.Kuna milima kama kimange, magana,misisya na keswa.Kuna koo kubwa za Warimba, Washora na Waruhu. 0784436058
| Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wakabwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |