Ramadan (mwezi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ramadan (Kiar. رمضان) (pia: ramadhani, ramazani) ni mwezi wa tisa katika Kalenda ya Kiislamu na mwezi wa kufunga katika Uislamu.

Mwislamu mzima mwenye afya nzuri anatakiwa kushiriki katika swaumu ambayo ni ibada ya kufunga chakula na kinywaji mchana wote.

Mwisho wa Ramadan ni sikukuu ya Idul Fitri (عيد الفطر - ʿīdu ʾl-fiṭr) ambayo ni sherehe ya furaha na kupongezana. Wailsmu hutoa zakat (zakatul-fitri زكاة الفطر) na kusali baadaye hukutana kwenye karamu.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ramadan (mwezi) kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.