Zaka
Zaka ni toleo la sehemu ya mapato ambalo muumini wa dini fulani anapaswa kutoa.
Yaliyomo |
Katika Biblia [hariri]
Desturi ya Mashariki ya Kati ya kutoa sehemu moja ya kumi kwa makuhani iliingia katika Uyahudi kuanzia Abrahamu aliyempa Melkisedek mfalme wa Salem aliyekuwa pia kuhani wa El Elyon (Mungu Mkuu).
Habari hiyo inasimuliwa katika Kitabu cha Mwanzo 14:18-20 na kusisitizwa na Waraka kwa Waebrania 7:5.
Zaka inaagizwa na vitabu vya Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Sheria.
Baadaye wajibu huo ulisisitizwa na Kitabu cha Malaki 3:8-12 na Kitabu cha Tobiti 1:6–8.
Katika Agano Jipya, mtume Paulo alifundisha kuwa anayetumikia kwenye altare anastahili kupata riziki zake kwa njia hiyo (Waraka wa kwanza kwa Wakorintho 9:13).
Katika Ukristo [hariri]
Mwanzoni waamini walikuwa wanawajibika, lakini baadaye zilianza kutolewa sheria ili kuwahimiza, kwa mfano katika mtaguso wa Tours (567) na ule wa Mâcon (585).
Hatimaye Papa Adrian I alipitisha maagizo hayo mwaka 787.
Baadaye njia za kuwategemeza viongozi wa Kanisa zilitofautiana kadiri ya nchi na madhehebu.
Katika Uislamu [hariri]
Zakat (kwa Kiarabu زكاة, yaani "kutoa msaada"), ni mojawapo ya Nguzo Tano za Kiislamu, ambayo inadai muumini atoe sehemu fulani ya mapato yake kwa maskini.
Tendo hilo muhimu linatazamwa na Waislamu kama njia ya kujipatia utakaso wa uroho na ubinafsi na ya kubarikiwa katika riziki zao.
Katika Usingasinga [hariri]
Katika dini ya Sikh muumini anadaiwa kutoa dasvand (ਦਸਵੰਦ) maana yake moja kwa kumi. Inaonekana sheria hiyo ilitokana na Uislamu.