Mwanaanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanaanga Piers Sellers nje ya chombo cha space shuttle tarehe 12 Juni 2006.

Mwanaanga ni mtu anayerushwa katika anga-nje yaani anga lililo nje ya angahewa ya dunia. Majina mengine yaliyokuwa kawaida ni "kosmonauti" (kwa Kirusi: космонавт) kwa wanaanga Warusi na "astronauti" (kwa Kiingereza astronaut) kwa wanaanga kutoka Marekani. Wachina wametumia neno "taikonauti".

Mwanaanga wa kwanza katika historia ya binadamu alikuwa Mrusi Yuri Gagarin kutoka Umoja wa Kisovyeti aliyerushwa tarehe 12 Aprili 1961 kwa chombo cha angani Vostok akizunguka dunia yote mara moja katika muda wa dakika 108.

Alifuatwa tarehe 5 Mei 1961 na Alan Shepard kutoka Marekani aliyetumia chombo cha angani cha Mercury .

Mwanamke wa kwanza angani alikuwa Mrusi Valentina Tereshkova mwaka 1963.

Wanaanga wa kwanza waliofika kwenye uso wa Mwezi walikuwa Wamarekani Neil Armstrong na Buzz Aldrin tarehe 20 Julai 1969.

Hadi Machi 2008 jumla ya watu 477 kutoka nchi 39 walifika kwenye kimo cha kilomita 100 juu ya uso wa dunia ambacho ni kimo ambako anga-nje linaanza kulingana na maelezo ya Shirikisho la Kimataifa kwa Usafiri wa Angani (Fédération Aéronautique Internationale (FAI)).

Kati ya hawa ni 24 waliofika mbali kuliko kilomita 2,000 juu ya uso wa dunia hadi njia ya mwezi kwenye anga.

Mwanaanga aliyekaa muda mrefu angani alkuwa Mrusi Sergei Krikalyov aliyefika angani mara sita akakaa jumla ya siku 803, saa 9 na dakika 39 kwenye anga-nje.

Baina ya miaka 2001 hadi 2009 watu saba walifika kwenye anga-nje kama watalii yaani wageni waliolipia nafasi ya kusafiri pamoja na wanaanga hadi Kituo cha Anga cha Kimataifa (ISS) walipokaa kwa wiki moja. Walilipa zaidi ya dolar milioni 20. Mmojawao alikuwa Mark Shuttleworth wa Afrika Kusini.

Picha za wanaanga

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanaanga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.