Yuri Gagarin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Yuri Gagarin mwaka 1963.

Yuri Alexeyevich Gagarin (kwa Kirusi Юрий Алексеевич Гагарин; 9 Machi 1934 huko Klushino karibu na Smolensk, Urusi - 27 Machi 1968) alikuwa mwanaanga wa kwanza katika historia yaani mtu wa kwanza aliyefika kwenye Anga-nje.

Alimwoa Valentina Goryachova akawa na mabinti wawili ambao ni Galina na Yelena. Akajiunga na Jeshi la Anga ya Urusi mwaka 1955.

Mwaka 1960 aliteuliwa katika kikosi cha kwanza cha marubani walioandaliwa kurushwa kwa anga-nje akateuliwa kuwa mtu wa kwanza wa kutoka duniani.

Tarehe 12 Aprili 1961 alirushwa na chombo cha angani Vostok 1 akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108.[1]

Alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa kituo cha kuandaa wanaanga Warusi. Mwaka 1968 alikufa katika ajali ya ndege alipofanya mazoezi ya urubani akazikwa kwenye makaburi ya heshima huko Moscow.

Kuhusiana na kifo Cha Gagarin, maombolezo ya kitaifa yalitangazwa katika Umoja wa Kisovyeti (kwa mara ya kwanza katika historia ya USSR kwa kumbukumbu ya mtu ambaye hakuwa mkuu wa nchi). Kwa heshima ya cosmonaut ya Kwanza Ya Dunia, idadi ya makazi yalipewa jina, barabara na njia zilipewa jina. Makaburi mengi ya Gagarin yamejengwa katika miji tofauti ya ulimwengu.

Stempu na sarafu[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yuri Gagarin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Wilson, Jim (2011-04-13). Yuri Gagarin: First Man in Space (en). NASA. Jalada kutoka ya awali juu ya 2023-03-14. Iliwekwa mnamo 2023-03-27.