Mbuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mbuni
Mbuni Somali
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Struthioniformes (Ndege kama mbuni)
Familia: Struthionidae (Ndege walio na mnasaba na mbuni)
Jenasi: Struthio
Linnaeus, 1758
Spishi: Angalia katiba

Mbuni ni ndege wakubwa wa familia Struthionidae. Kuna spishi mbili katika jenasi moja, lakini wataalamu wengine wanafikiri ni spishi moja tu. Ndege hawa ni wakubwa kuliko wengine wote. Wana miguu mirefu na shingo refu na wanaweza kukimbia sana, hata kwa mwendo wa km 65 kwa saa, lakini hawawezi kuruka angani. Mbuni wanaishi savana na nyika na majangwa ya Afrika, lakini wanafugwa ulimwengu wote. Jina la sayansi la spishi kuu, Struthio camelus, linatoka lugha ya Kiyunani: στρουθιον = jurawa na καμηλος = ngamia.

[hariri] Spishi

Usambazaji wa mbuni kwa Afrika

[hariri] Spishi za kabla ya historia

  • Struthio anderssoni - spishi kutoka mayai(?)
  • Struthio asiaticus (Asian Ostrich) (Asia ya kati mpaka China, mwanzo wa Pliocene - mwisho wa Pleistocene)
  • Struthio brachydactylus (Ukraine, Pliocene)
  • Struthio chersonensis (Ulaya wa kusini mashariki mpaka Asia ya magharibi ya kati, Pliocene) - spishi kutoka mayai
  • Struthio coppensi (Elizabethfeld, Namibia, mwanzo wa Miocene)
  • Struthio daberasensis (Namibia, mwanzo - kati ya Pliocene) - spishi kutoka mayai
  • Struthio dmanisensis (Dmanisi, Georgia, mwisho wa Pliocene/mwanzo wa Pleistocene)
  • Struthio kakesiensis (Laetoli, Tanzania, mwanzo wa Pliocene) - spishi kutoka mayai
  • Struthio karingarabensis (Afrika ya kusini magharibi na kati, mwisho wa Miocene - mwanzo wa Pliocene) - spishi kutoka mayai(?)
  • Struthio linxiaensis (Yangwapuzijifang, China, mwisho wa Miocene)
  • Struthio oldawayi (Tanzania, mwanzo wa Pleistocene - labda spishi ndogo ya S. camelus)
  • Struthio orlovi (Moldavia, mwisho wa Miocene)
  • Struthio wimani (China na Mongolia, mwanzo wa Pliocene)


[hariri] Picha