Kiyunani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kiyunani - jina hilo ni la Kiswahili cha zamani kwa "Kigiriki", ambayo ni lugha ya nchi ya Ugiriki ("Uyunani") au tabia za Wagiriki ("Wayunani").

Neno la Kiswahili cha zamani limetokana na lugha ya Kiarabu يونان yunan na hapa ilitaja kiasili Wagiriki wa eneo la Ionia au wa kabila la Ioni walioishi kwenye pwani la mashariki la Bahari ya Aegeis.

Leo hii si kawaida sana lakini inapatikana hasa katika matoleo mbalimbali ya Biblia. Miaka ya nyuma neno la "Kigiriki" likasambaa zaidi, kutokana na athira ya Kiingereza kinachotumia maneno "Greece, Greek" kutoka Kilatini "Graeci" ambayo ni kawaida katika lugha nyingi za Kiulaya. Wanaotajwa wenyewe hujiita "Helleni", lugha yao "Helleniki".