Ngamia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ngamia
Ngamia nundu-moja
Ngamia nundu-moja
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Tylopoda
Familia: Camelidae (Wanyama walio na mnasaba na ngamia)
Jenasi: Camelus (Ngamia)
Linnaeus, 1758
Spishi: Camelus dromedarius (Ngamia nundu-moja)

Camelus bactrianus (Ngamia nundu-mbili)

Ngamia ni jenasi ya mamalia wakubwa wa familia ya Camelidae inayowajumlisha pamoja na lama (mnyama) na vikunya wa Amerika Kusini.

Kuna spishi mbili za ngamia:

Makazi[hariri | hariri chanzo]

Spishi zote mbili wamezoea kuishi katika mazingira yabisi kama jangwa au nusu jangwa.

Ngamia nundu moja anapatikana katika Uarabuni, Mashariki ya Kati hadi Pakistan, Afrika ya Kaskazini, Somalia na kaskazini ya Kenya. Wakati wa karne ya 19 walipelekwa Australia walipozoea haraka kwa sasa wako mnamo 300,000. Spishi hii inavumilia joto kali lakini pia baridi za usiku kwenye Sahara. Anaweza kubadilisha halijoto ya mwilini kati ya sentigredi 34 na 41 kulinana na maingira.

Ngamia wa Asia yuko katika kanda kuanzia Anatolia hadi Manchuria katika kaskazini ya China. Amezoea zaidi baridi ya Asia ya Kati; wakati wa majira barafu halijoto ya mazingira inafikia -30°C. Joto kali inampa matatizo kidogo na kumchelewesha.

Spishi zote mbili zinakutana katika nchi kuanzia Uturuki, Uajemi, Afghanistan hadi Pakistan.

Mwili[hariri | hariri chanzo]

Maumbile yao yamelingana na mazingira ya jangwani. Miguu ni mapana na kuzuia wasizame chini kwenye mchanga. Nywele ni ndefu zinakinga dhidi ya joto na baridi.

Nundu ni mahali pa stoo ya akiba ya mafuta; kama ngamia inapita pasipo na chakula inatumia mafuta kwa nishati ya mwilini haihitaji kula kwa kipindi hadi siku 30.

Wanaweza kushika lita 100-150 mwilini na kuendelea jangwani bila kunywa maji kwa wiki 2. Penye majani mabichi ya kutosha na kama joto sio kali mno ngamia anaweza kuendelea bila kunywa kwa wiki kadhaa.

Shingo ni ndefu kwa sababu kwa chakula anapendelea majani ya miti na vichaka.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Ngamia wa Asia (C. bactrianus) ana nundu mbili

Ngamia ni wanyama wa kijamii na kiasili hushi katika kundi za dume mmoja na jike kadhaa. Siku hizi kuna Ngamia wa Asia mamia kadhaa kwenye pori ambao ni mabaki wa ngamia pori wa zamani. Wako China na Mongolia. Ngamia nundu moja hakuna wanyama wa pori asilia tena; inaaminiwa walitokea Uarabuni kiasili. Lakini kuna wanyama waliotoroka huko Australia na Amerika wanaoishi peke yao hawafugwi.


Ngamia na binadamu[hariri | hariri chanzo]

Ngamia wamefugwa na binadamu tangu miaka 5,000 - 6,000. Leo hii kuna takriban wanyama hawa milioni 19 na idadi kubwa yaani milioni 14 wako Afrika, milioni saba pekee nchini Somalia na milioni 3.3 nchini Sudan.

Watu hufuga ngamia kwa kubeba watu na mizigo. Nywele zao ni aina ya sufi inayotumiwa kutengeneza shuka, hema na pia vitambaa vya nguo. Wanachinjwa kwa nyama yao.

Ngamia hukamuliwa pia kama ng'ombe. Katika nchi yabisi kiasi cha maziwa yanalingana na ng'ombe. Katika miaka ya nyuma Wamassai wa Kenya na pia Tanzania wameanza kufuga ngamia baada ya kuona ya kwamba ng'ombe zao walikufa wakati wa ukame lakini ngamia wameendelea kuishi na kutoa maziwa. Ngamia anachukua chakula chake kwenye mti mwenye mizizi mirefu kushinda manyasi yanayoliwa na ng'ombe. Kwa sababu hiyo manyasi kukauka haraka wakati wa ukame kuliko majani ya miti.


Gallery[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Crystal Clear app babelfish.png Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngamia kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.