Exit 13

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Exit 13
Exit 13 Cover
Studio album ya LL Cool J
Imetolewa 9 Septemba 2008
Imerekodiwa 2007–2008
Aina Hip hop
Urefu 72:43
Lebo Def Jam
Mtayarishaji LL Cool J (exec.)
Suits & Ray Burghardt, Ryan Leslie, Illfonics, The Dream Team, DJ Scratch, Frado & Absolut, Tricky Stewart, Raw Uncut, Marley Marl, Cue Beats, Dame Grease, Music Mystro, StreetRunner
Tahakiki za kitaalamu
Wendo wa albamu za LL Cool J
Todd Smith
(2006)
Exit 13
(2008)
All World 2
(2009)
Single za kutoka katika albamu ya Exit 13
  1. "Rocking with the G.O.A.T."
    Imetolewa: 20 Juni 2008
  2. "Baby"
    Imetolewa: 1 Julai 2008
  3. "Feel My Heart Beat"
    Imetolewa: 26 Agosti 2008

Exit 13 ni albamu ya kumi na mbili (ya 13 kwa ujumla) na albamu ya mwisho ya LL Cool J kujihusisha na studio ya rekodi ya Def Jam Recordings, uhusisho ambao ulidumu kwa takriban miaka kumi na miwili. Awali albamu ilipewa jina la Todd Smith Pt. 2: Back to Cool. Albamu ilitolewa mnamo tar. 9 Septemba 2008.

Matayarisho[hariri | hariri chanzo]

Albamu ni ya kwanza kwa albamu za LL Cool J tangu G.O.A.T. kuwa na nembp ya parental advisory kwa mashairi makali. Kwenye mahojiano ya redio yaliyofanywa na DJ Z kule mjini Chicago, LL alisema kwamba maneno yasiyo ya adabu si mabaya sana. Badala ya kutoimba maneno haya mabaya, toleo lililohaririwa linatumia mashairi mengine badala ya yale yasiyo ya adabu.[1] LL na DJ Kayslay wameungana ili kuweza kutoa albamu yao ya kwanza ya mixtape ukiwa kama utangulizi wa jina la Exit 13 liopewa jina la The Return of the G.O.A.T..

Wachangiaji wengie wa katika albamu hii ni pamoja na 50 Cent, Sheek Louch, Fat Joe, Ryan Leslie, Wyclef Jean, The-Dream, Lil Mo, Grandmaster Caz, Funkmaster Flex, Richie Sambora na Darlisa Blackshere.

Single[hariri | hariri chanzo]

Toleo lisilo rasmi la single ya mtaani, "Rockin' with the G.O.A.T.," ilianza kutolewa kwa mara ya kwanza mnamo tar. 20 Juni 2008.

Toleo rasmi la single ya kwanza, "Baby" akimshirikisha The-Dream ilitolewa mnamo tar. 1 Julai 2008 kupitia Maduka ya Muziki ya iTunes. Mnamo tar. 19 Agosti 2008, iTunes wametoa remixi ya ya rock akimshirikisha Richie Sambora, ikiwa na mahadhi ya rock na mistari ya kasi kidogo.

Toleo rasmi la single ya pili, "Feel My Heart Beat" akimshirikisha 50 Cent ilitolewa mnamo tar. 26 Agosti 2008. Lakini kwa bahati mbaya wimbo haukiingia katika chati za Billboard Hot 100. Toleo rasmi la wimbo huo ulivuja kwenye mtandao wa intaneti mnamo tar. 27 Novemba 2008.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

# Jina Mtayarishaji Wageni walioshirikishwa Muda
1 "It's Time for War" Suits & Ray Burghardt 5:06
2 "Old School New School" Ryan Leslie 3:41
3 "Feel My Heart Beat" The Dream Team 50 Cent 3:21
4 "Get Over Here" Frado & Absolut It's Ya Girl Nicolette, Jiz, Lyrikal, & Ticky Diamondz 5:49
5 "Baby" Tricky Stewart The-Dream 4:01
6 "You Better Watch Me" Marley Marl & M.Will 4:20
7 "Cry" Raw Uncut Lil' Mo 4:15
8 "Baby (Rock Remix)" Suits & Ray Burghardt Richie Sambora 3:08
9 "Rocking with the G.O.A.T." DJ Scratch 3:43
10 "This Is Ring Tone M..." DJ Scratch Grandmaster Caz 2:52
11 "Like a Radio" Ryan Leslie Ryan Leslie 3:34
12 "I Fall in Love" Suits & Ray Burghardt Élan of the Dey 3:57
13 "Ur Only a Customer" Dame Grease & Music Mystro 2:18
14 "Mr. President" Suits & Ray Burghardt Wyclef Jean 4:35
15 "American Girl" Illfonics Mark Figueroa 4:26
16 "Speedin' on da Highway/Exit 13" Suits & Ray Burghardt Funkmaster Flex 4:49
17 "Come and Party with Me" Illfonics Fat Joe & Sheek Louch 4:37
18 "We Rollin'" Cue Beats 3:03
19 "Dear Hip Hop" StreetRunner 4:28
20 "New York, New York (Interlude)"
(Japanese & iTunes Bonus Track)
Kander and Ebb 0:18
21 "New York"
(Japanese & iTunes Bonus Track)
Suits & Ray Burghardt 4:28

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (2008) Nafasi
iliyoshika
Canadian Albums Chart[2] 61
U.S. Billboard 200[3] 9
U.S. Billboard Top R&B/Hip-Hop Albums[4] 3
U.S. Billboard Top Rap Albums[4] 2

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. LL Cool J interview on DJBooth.net. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-05-30. Iliwekwa mnamo 2010-02-06.
  2. HMV Canada: "All Hope is Gone" by Slipknot tops CD sales list. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-09-12. Iliwekwa mnamo 2010-02-06.
  3. Slipknot Edges The Game Atop Billboard 200. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-21. Iliwekwa mnamo 2010-02-06.
  4. 4.0 4.1 http://www.mtv.com/news/articles/1593987/20080903/slipknot.jhtml