10 ni jina la kutaja albamu ya tisa ya rapa wa Kimarekani, LL Cool J. Albamu ilitolewa mnamo tar. 15 Oktoba, 2002 na studio za Def Jam Recordings. Albamu iliweza kushika chati nafasi ya pili katika chati za Billboard 200 huko nchini Marekani. LL Cool J na 10 amefikisha lengo la Def Jam katika historia, kwa kuwa msanii msanii wa kwanza kuwa na albamu kumi kwenye Def Jam (mbali na mpango mzima wa albamu kumi na tatu) akiwa chini ya studio moja.