Ebola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Picha ya virusi cha Ebola jinsi kinavyoonekana kwenye hadubini ya elektroni

Ebola, inatamkwa E- Bo-la, ni virusi vya homa ya hemoraji (ugonjwa wa damu kutoganda). (Hemorrhagic inamaanisha "kumwaga damu kwa sana".) Ni ugongwa unaoua sawa. Katika orodha ya watu 10 waliopata virusi cha Ebola, basi wastani kati ya watano au tisa hufa. Watu walioambukizwa virusi cha Ebola hupata Homa ya Ebola ya hemorrhagic.

Namna watu wanavyopata Ebola[hariri | hariri chanzo]

Katika watu, hutoa maambukizi kwa watu pale inapotokea anagusa ugiligili wenye virusi. Ebola haiwezi kupatikana kwa njia ya hewa. Watu wenye Ebola hupata homa ya kumwaga damu kwa sana. Uhara damu na kutapika. Wanamwaga damu kutoka puani, mdomoni, katika viungo vya uzazi. Uvujaji huu unaweza kuambukiza kwa haraka sana (unaweza kusababisha watu wengine wapate virusi.)

Dalili za Ebola[hariri | hariri chanzo]

Pale watu wanapopata Ebola, dalili zake za kwanza ni kuonekana kama magonjwa mengine. Watu wanapata homa, kujisikia kuchoka, maumivu ya kichwa, maumivu ndani ya tumbo, maumivu katika viungo vyao, na maumivu ya kooni. Kwa dalili hizi, watu hufikiria kwamba wana magonjwa mengine kama vile malaria au homa ya matumbo.

Baadaye, hali inakuwa mbaya zaidi. Kiasi kufikia hali ya kumwaga damu kwa kiasi kikubwa sana. Wanapata mshituko: shinikizo la damu kuwa chini, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi, na mzunguko wa damu kuwa hafifu mwilini. Hii inasababisha viungo vya mwili kuuma sana. Viungo vya mwili vinaacha kufanyakazi. Ebola pia husababisha ukakamavu mwilini ambapo inamwacha waathirika kitandani. Hata kama watafanikiwa kufika hospitalini, lakini wengi wao hufa.

Tiba ya Ebola[hariri | hariri chanzo]

Hakuna tiba maalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu wanapata huduma bora kutoka kwa madaktari na wauguzi, wengi wao huishi. Huduma bora kwao inaweza kuwa kwa ugiligili au damu zinazotolewa kwa vena za watu. Inaweza kuwa dawa za kufanya shinikizo la damu na mzunguko wa damu ufanyekazi vizuri.

Ebola huhesabiwa moja kati ya magonjwa ya mlipuko. Wagonjwa wa Ebola hutengenishwa na wagonjwa wengine ili wasipate kuambukizwa. Hii ina-maana kwamba ugiligili na damu wasije watu wengine wakagusa. Basi watu wengine hawawezi kupata virusi hivi kwa sababu tayari hatua ya kuwatenganisha ishapita.

Pale mlipuko unapotokea, watu wengi huja na kujaribu kusaidia kuzuia. Shirika la Afya Duniani ni moja kati ya kundi muhimu sana kwa jitahada zake za kujaribu kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Bibliografia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]