Homa ya matumbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Homa ya matumbo husababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhi. Ugonjwa huu huambukizwa kwa mtu kula au kunywa chakula au maji yalio na kinyesi cha mu aliyambukizwa.[1] Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye matumbo ya binadamu.

Mgonjwa wa homa ya matumbo aliye na vitone vyekundu kwa ajili ya bakteria wa Salmonella

Yaliyomo

[hariri] Dalili

  • Homa kali
  • Kutoka kwa majasho mengi
  • Kuharisha (bila ya kutoa damu)
  • Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana kwenye mwili.

Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.

Katika wiki ya kwanza:

  • Joto la mwili huongezeka
  • Kichwa huuma
  • Kukohoa
  • Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa ni nadra kutokea.
  • Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea

Katika wiki ya pili:

  • Homa huongezeka
  • Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
  • Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
  • Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au nane kwa siku.
  • Kutapika kwa mgonjwa
  • Ini la mgonjwa huvimba
  • Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.

Wiki ya tatu:

  • Matumbo hutoa damu.
  • Matumbo hutoboka

Wiki ya tatu ikimalizika, homa huanza`kutilia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.

[hariri] Matibabu

Mara nyingi, homa ya matumbo haiuwi binadamu. Dawa kama ampicillin, chloramphenicol, trimethoprim-sulfamethoxazole, Amoxicillin and ciprofloxacin hutumika kutibu wagonjwa katika nchi zilizoendelea.

[hariri] Hatua za kuzuia kupata homa hii

Daktari akimpa mtu chanjo mjini San Augustine County, Texas
  • Usafi wa mazingara na wa kibinafsi ni hatua bora ya kujikina kutokamana na ugonjwa huu.
  • Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hivyo maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
  • Homa hii hueza kuenea kwenye mazingara ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
  • Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa majina Typhim Vi iliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherix iliyotengenezwa na GlaxoSmithKline.

[hariri] Historia

Mnamo mwaka 2004-05, janga la homa ya matumbo lilizuka katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoathiri watu 42,000 na kuuwa watu 214 (kulingana na ripoti ya shirika la World Health Organisation).

[hariri] Waathiriwa maarufu

  • Mary Mallon, aliyejulikana kama Typhoid Mary.
  • Louisa May Alcott, mwandishi wa Little Women.
  • Charles Darwin, mwanasayansi, aliathirika pindi alipoenda nchini Chile mnamo 1835.
  • Eugenia Tadolini, alikufa mjini Paris mnamo 1872.
  • William Wallace Lincoln, mtoto wa tatu wa Abraham Lincoln, ambaye ni rais wa 16 wa Marekani, pamoja na Mary Todd Lincoln, walifariki kutokana na maradhi haya mnamo February 20, 1862.
  • Wilbur Wright, alikufa mnamo May 30, 1912 baada ya kuugua homa hii.

[hariri] Marejeo

  1. Giannella RA (1996). "Salmonella", Baron's Medical Microbiology (Baron S et al., eds.), 4th, Univ of Texas Medical Branch. ISBN 0-9631172-1-1. 

[hariri] Kusoma zaidi

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine