Zeno wa Verona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Zeno alivyochorwa katika karne XIV.
Sanamu ya "San Zen che ride" ("Mtakatifu Zeno akicheka") katika basilika lake huko Verona.

Zeno wa Verona (300 - 371) alikuwa askofu wa nane wa Verona (Italia) kuanzia mwaka 362.

Anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa katika sikukuu yake tarehe 12 Aprili au 21 Mei.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Hakuna habari nyingi za hakika kuhusu maisha yake, lakini inaonekana alitokea Mauretania (Afrika kaskazini) akiwa msomi.

Zimetufikia hotuba zake 16 ndefu na 77 fupi, zinazoonyesha alivyopambana na Upagani na uzushi wa Ario.