Nenda kwa yaliyomo

Yohane wa Nepomuk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Yohane wa Nepomuk.
Kifodini cha Mt. Yohane wa Nepomuk kilivyochorwa na Szymon Czechowicz, National Museum in Warsaw, Polandi.

Yohane wa Nepomuk (kwa Kicheki: Jan Nepomucký; kwa Kijerumani: Johannes Nepomuk; kwa Kilatini: Ioannes Nepomucenus[1]; Nepomuk, 1345 hivi – Prague, 20 Machi 1393[2]) alikuwa padri wa Bohemia (leo nchini Ucheki). Aliuawa kwa kutoswa mtoni Vltava kutoka darajani kwa agizo la mfalme Wenseslaus IV, mfalme wa Warumi na wa Bohemia.

Baadaye ilisimuliwa kwamba alikuwa muungamishi wa malkia na kwamba alikataa ombi la mfalme la kutoboa siri za kitubio. Kwa msingi huo anahesabiwa kama mfiadini wa kwanza wa siri ya kitubio na msimamizi dhidi ya masingizio.[2]

Alitangazwa mwenye heri tarehe 31 Mei 1721, halafu Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 19 Machi 1729.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 20 Machi[3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Sanctus Johannes Nepomucenus Christi Heiliger Blut-Zeug. 1723.
  2. 2.0 2.1 Krčmář, Mgr. Luděk. "Saint John of Nepomuk". SJN.cz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-02-21. If in 1369 John of Pomuk was a notary public, he must have been more than twenty years old. Thus he was probably born sometimes between 1340 and 1350 [1349].
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.