Nenda kwa yaliyomo

Yohane Yosefu wa Msalaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sura ya Mt. Yohane Yosefu

Yohane Yosefu wa Msalaba (Ischia, 15 Agosti 1654 - Napoli, 5 Machi 1734) alikuwa padri wa shirika la Ndugu Wadogo Pekupeku kutoka Italia aliyependa sana ufukara hata akavaa kanzu ileile miaka 64 akaitwa "padri virakamia".

Akifuata nyayo za Petro wa Alcantara, alirekebisha konventi nyingi za Wafransisko wa mkoa wake.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Kwanza alitangazwa mwenye heri mwaka 1789, halafu mtakatifu mwaka 1839 na Papa Gregori XVI.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.