Nenda kwa yaliyomo

Yohane Nepomuk Neumann

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Yohane katika mavazi ya kiaskofu.

Yohane Nepomuk Neumann, C.Ss.R. (Prachatice[1], Austria-Hungaria [2], 28 Machi 1811Philadelphia, Marekani, 5 Januari 1860) alikuwa Mkristo wa Bohemia (Ucheki) aliyehamia Marekani mwaka 1836 ili aweze kupata upadrisho[3], akapewa baada ya wiki tatu tu.

Halafu akajiunga na Waredentori ili kufaidika na maisha ya kijumuia (1840)[4] na hatimaye akawa askofu mkuu wa Philadelphia (1852–1860). Katika jimbo kuu hilo aliunda mfumo wa shule wa kijimbo wa kwanza nchini Marekani: chini yake kutoka 1 tu, shule zake zikawa 200. Pamoja na kushughulikia sana malezi ya watoto, aliwajibika kwa hali na mali kwa ajili ya umati wa wahamiaji fukara[5].

Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Oktoba 1963 na mtakatifu tarehe 19 Juni 1977[6] , mwanamume wa kwanza (na hadi sasa wa pekee) raia wa nchi hiyo[7].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[8].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Die Böhmerwälder Wurzeln des Heiligen Johann Nepomuk Neumann" (PDF). Iliwekwa mnamo Machi 4, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "About St. John Neumann". The National Shrine of St. John Neumann. Iliwekwa mnamo Januari 5, 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Saint John Neumann". loyolapress.com. Iliwekwa mnamo Septemba 19, 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "History". historicalalphonsus.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-06. Iliwekwa mnamo Mei 2, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Martyrologium Romanum
  6. Canonization of John Nepomucene Neumann, Homily of Paul VI, Sunday, 19 June 1977 vatican.va
  7. "History". staugustinechurch.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 19, 2015. Iliwekwa mnamo Septemba 19, 2015.
  8. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.