Wimbi la Njaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Hili Game"
"Hili Game" kava
Wimbo wa Juma Nature

kutoka katika albamu ya Nini Chanzo

Umetolewa 2000/2001
Umerekodiwa 2000
Aina ya wimbo Hip hop
Urefu 3:40
Studio Bongo Records
Mtunzi Juma Nature
Mtayarishaji P. Funk
Nini Chanzo orodha ya nyimbo
  1. "Kighettoghetto"
  2. "Sonia"
  3. "Wimbi la Njaa" (remix 2001)
  4. "Jinsi Kijana"
  5. "Tumepigika"
  6. "Nini Chanzo"
  7. "Juu kwa Juu"
  8. "Hili Game"
  9. "Jinsi Kijana" (remix)
  10. "Haya We"
  11. Wimbi la Njaa (orijino 2000)

"Wimbi la Njaa" ni jina la wimbo wa Juma Nature akiwa na kundi lake la F.S.G kutoka Temeke, Dar es Salaam, Tanzania. Wimbo umetoka mwaka 2000. Wimbo huu ni wimbo wa pili kurekdi akiwa na F.S.G na umepata kuonekana kwenye tepu ya kwanza ya albamu ya Juma Nature Nini Chanzo. Baadaye ukaja kufanyiwa remix akiwa na KR Mullah na kuwekwa katika albamu tu. Wakati huu muziki kutoka TMK ulikuwa unapamba moto. Juma Nature aliinua TMK vya kutosha kuanzia 2000 hadi 2006. Ngoma kibao alipata kushirikishwa na wasanii wengi kutoka TMK na wengine mahali pengine pa Dar.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


Kigezo:Juma Nature