Nini Chanzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nini Chanzo
Nini Chanzo Cover
Studio album ya Juma Nature
Imetolewa 2001
Aina Hip hop
Lebo Bongo Records
Mtayarishaji P. Funk
Tahakiki za kitaalamu
  • Rating-Your-Music 3.5/5 stars [1]
Wendo wa albamu za Juma Nature
Nini Chanzo
(2001)
Ugali
(2004)
Single za kutoka katika albamu ya Nini Chanzo
  1. "Jinsi Kijana"
    Imetolewa: 2001
  2. "Kighettoghetto"
    Imetolewa: 2001
  3. "Sonia"
    Imetolewa: 2001
  4. "Hili Game"
    Imetolewa: 2001


Nini Chanzo ni jina la kutaja albamu ya kwanza ya msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Juma Nature. Albamu ilitolewa mwaka wa 2001 ikiwa imetayarishwa chini ya P. Funk Majani lakabu Kinyewele Kimoja. Albamu ilisambazwa na Wananchi Stores ya Dar es Salaam. Hii ni albamu ya kwanza ya Nature tangu aingie katika tasnia ya muziki, na ndiyo mwanzo wa albamu bora za baadaye.

Albamu imeshirikisha wasanii kibao ikiwa ni pamoja na T.I.D katika Hili Game kaimba kiitikio, A.Y. katika "Tumepigika", Mr. Paul katika Kighettoghetto, KR Mullah katika "Wimbi la Njaa Remix 2001 (upo katika albamu tu), Mack D. katika "Haya We" na wengine kibao.

Ni moja kati ya albamu za hip hop za miaka ya 2000 za muda wote.

Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya nyimbo zilizopo katika albamu hii.

  1. Kighettoghetto
  2. Sonia
  3. Wimbi la Njaa (remix 2001)
  4. Jinsi Kijana
  5. Tumepigika
  6. Nini Chanzo
  7. Juu kwa Juu
  8. Hili Game
  9. Jinsi Kijana (remix)
  10. Haya We
  11. Wimbi la Njaa (orijino 2000)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]