Wagadugu
Mandhari
Jiji la Wagadugu | |
Nchi | Burkina Faso |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 2,453,496 |
Wagadugu (kwa Kifaransa huandikwa Ouagadougou) ni mji mkuu wa Burkina Faso, na pia mji mkubwa kabisa wa nchi hiyo na wa mkoa wa Centre.
Mwaka 2019 idadi ya wakazi ilikuwa milioni 2,453,496, lakini mji unakua haraka.
Wagadugu iko katika jimbo la Kadiogo. Kuna ofisi za serikali na viwanda kadhaa vya nguo na vyakula.
Mji ni pia kitovu cha usafiri na mawasiliano. Kuna kiwanja cha kimataifa cha ndege na njia ya reli kwenda Abidjan (Côte d'Ivoire), halafu barabara za kwenda Lome (Togo), Bamako (Mali), Niamey (Niger), Accra (Ghana).
Wagadugu ina chuo kikuu kilichokuwa chuo cha mwanahistoria maarufu Joseph Ki-Zerbo.
Tamasha la kimataifa la filamu za Afrika (FESPACO) hufanyiwa Wagadugu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wagadugu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |