Visiwa vya South Georgia na South Sandwich
Visiwa vya South Georgia na South Sandwich ni eneo la ng'ambo la Uingereza kusini mwa Bahari Atlantiki.
Eneo hilo ni mafunguvisiwa mawili ya South Georgia na South Sandwich, halafu visiwa vingine vidogo sana vilivyosambaa katika maeneo mapana ya Atlantiki Kusini.
Visiwa vyote vina eneo la km² 3,900.
Idadi ya wakazi ni 20 na wengi wao ni wanasayansi wanaochunguza ndege wanaokaa kwenye visiwa pamoja na afisa mmoja mwakilishi wa serikali ya Uingereza.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Hakuna wenyeji kwenye visiwa hivi. Tangu karne ya 19 wavuvi wa nyangumi kutoka Ulaya walijenga huko vituo ambako walipeleka nyangumi kwa kuwakatakata na kupika mafuta yao. Vituo hivyo vilikuwa na makumi hadi mamia ya wakazi wakati wa kuwinda nyangumi lakini wakati wa baridi ni watu wachache tu waliobaki. Vituo hivyo vilifungwa katika miaka ya 1960 kutokana na kupotea kwa nyangumi.
Mwaka 1904 mvuvi kutoka Norwei alianzisha kijiji cha Grytviken kama kituo cha kupikia mafuta ya nyangumi na kijiji hicho ni makazi pekee ya kudumu kwenye visiwa hivi hadi leo.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Hadi mwaka 1985 eneo lilisimamiwa kutoka Visiwa vya Falkland lakini imepewa hadhi ya eneo la pekee. Ilhali hakuna wakazi wa kudumu pia hakuna baraza lililochaguliwa na mamlaka yote iko mikononi mwa afisa wa serikali ya Ufalme wa Muungano.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|