Usanifu wa ndani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mapambo ya Hoteli ya Bristol, Warsaw
Mapambo ya kale: Chuo cha Balliol, Oxford

Usanifu wa ndani ni sanaa na sayansi ya kuboresha muonekano wa ndani ya nyumba au jengo lolote, wakati mwingine ikiwa ni pamoja na nje, kufikia mazingira bora na yenye kupendeza kwa mtumiaji.

Msanifu wa ndani ni mtu ambaye anapanga, anatafiti, anaratibu, na kusimamia miradi ya upambaji wa ndani. Taaluma hii inajumuisha mambo kadhaa kama vile maendeleo ya dhana, mipangilio ya nafasi, ukaguzi, upangaji, utafiti, mawasiliano na wadau wa mradi, usimamizi wa ujenzi, na utekelezaji.

Katika siku za nyuma, usanifu wa ndani uliwekwa pamoja kwa kawaida kama sehemu ya mchakato mzima wa kujenga. Taaluma ya upambaji wa ndani imetokana na maendeleo ya jamii na usanifu wa majengo.

Katika India ya zamani, wasanifu wa majengo walifanya kazi kama wasanifu wa ndani. Hii inaweza kuonekana kutoka kwa marejeo ya Vishwakarma mbunifu - mmoja wa miungu katika hadithi za Uhindu.

Katika Misri ya kale, "nyumba za roho" au mifano ya nyumba ziliwekwa katika makaburi kama vipokea sadaka za chakula. Kutoka kwa haya, inawezekana kutambua maelezo juu ya usanifu wa ndani wa makazi tofauti katika falme tofauti za Misri, kama vile mabadiliko katika ujenzi wa viingiza hewa, nguzo, madirisha, na milango.

Mifano ya usanifu wa ndani[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usanifu wa ndani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.