Usalama wa kinyumbani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Usalama wa kinyumbani ni suala ibuka haswa katita miji na nchi ambapo kuna uwezekano mkubwa wa wizi, kuvunjwa nyumba na moto unaoweza ukateketeza kila kitu.

Usalama wa kinyumbani unahusisha mitambo ya kukagua kwamba kila kitu kiko shwari, kamera za CCTV, vihisia (sensors) vilivyoko milangoni na madirishani, ving'ora vitakavyolia pindi tu mwizi au moto utakapodhihirika.

Ripoti kutoka shirika la ukachero la FBI imeonyesha kwamba wizi mwingi, asilimia hamsini na nane hutokana na wezi kuvunja na kuingia nyumbani kwa fujo. Pia imeendelea kusema kwamba wizi hutokea kati ya dakika nane hadi kumi na mbili ambapo mwizi huwa ameingia nyumbani kwa kuvunja dirisha au mlango kwa muda usiozidi sekunde sitini.

Mitambo ya usalama wa kinyumbani[hariri | hariri chanzo]

Unapoweka usalama wa nyumbani mwako kupitia teknolojia hii mpya ya ADT Security, utahitaji kuweka kamera fiche za CCTV ambazo zitalinda usalama kwa kuangalia uwepo wa mwizi, mtu au kitu kigeni nyumbani. Licha ya kuweka kufuli au komeo dirishani na milangoni, utaweka pia vihisia ili kwamba mtu akiugusa mlango au dirisha yako, mtambo utakuonyesha kwamba kuna mtu pale.

Kando na hayo, utaweka king'ora ili kwamba kukiwa na tukio la kuvunjwa, kuguswa mlango au dirisha, moto au mwizi ameonekana na kamera ya CCTV, basi king'ora kitatoa mbiu ili ujue kwamba kuna hatari.

Kampuni ambayo yakupa usalama wa kinyumbani itakupa jopo la kudhibiti (control panel) ambayo utawekewa kwa simu au kompyuta ili uweze kudhibiti usalama wako.

Baada ya kampuni inayokupa usalama wa kinyumbani kufanya haya yote, wataviwasha viashiria kwa milango na dirishani ili kila mtu anayepitia pale ajue kwamba una usalama wa kutosha. Jambo hili hata kama laweza kuonekana kana kwamba ni jinsi ya uchuuzi, litawafanya wezi waogope kuvunja nyumba yako maana kwako kuna usalama wa kutosha.

Kamera za CCTV[hariri | hariri chanzo]

Kamera za CCTV ni mitambo ya kiusalama ambayo huwekwa ili kukagua kila kitu kilichoko mahali fulani. Huwa ni kamera ya kawaida lakini ambayo huona wakati wa mchana na usiku pia. Kamera hizi huambatanishwa na mtambo wa kukagua ambapo mkaguzi huweza kuona yote yanayojiri katika mahali panapokaguliwa na mtambo huu. Kamera hizi huwekwa nyumbani, na katika shule na ofisini kunakohitaji usalama wa hali ya juu. Tukio lolote likifanyika kama wizi au moto, wakaguzi wanaweza kujua haswa ni lipi lililojiri ili mkasa huo utokee.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  1. CCTV