Nenda kwa yaliyomo

Universal Zulu Nation

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Universal Zulu Nation ni kundi la kimataifa la uhamasishaji wa hip hop lilianzishwa na hapo awali liliongozwa na msanii wa hip hop Afrika Bambaataa.[1]: 101 

Nembo ya zamani ya Zulu Nation.

Universal Zulu Nation inakuza wazo la kwamba hip-hop ilianzishwa ili kudumisha maadili ya "amani, upendo, umoja na furaha" kwa watu wote bila kujali rangi, dini, au taifa.

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Afrika Bambaataa (kushoto) akiwa na DJ Yutaka wa Zulu Nation Japan, 2004.

Hapo awali kundi hili lilijulikana kwa jina la Organization, liliibuka miaka ya 1970 baada ya kubadilishwa kwa Black Spades, genge la mitaani kutoka eneo la South Bronx, New York. Ingawa Black Spades walikuwa msingi wa kundi hili, magenge mengine kama Savage Nomads, Seven Immortals, na Savage Skulls yalichangia wanachama zaidi. [2] Wanachama walianza kuandaa hafla za kitamaduni kwa ajili ya vijana, wakichanganya miondoko ya dansi na harakati za muziki katika kile ambacho sasa kinajulikana kama nguzo za utamaduni wa hip hop. Nguzo za utamaduni wa hip hop ni pamoja na Emceeing (MCing), Deejaying (DJing), breaking, na machata.

Katika mahojiano mengi, Afrika Bambaataa ameeleza kuwa jina "Zulu" lilitokana na filamu ya mwaka 1964 yenye jina kama hilo.

Taswira ya Zulu Nation imekuwa ikibadilika kwa nyakati tofauti. Wakati wa miaka ya 1970 na 1980, Afrika Bambaataa na wanachama wa Zulu Nation mara nyingi walivaa mavazi yanayowakilisha tamaduni za sehemu mbalimbali dunia na makundi mengine wanachama wa Zulu Nation dunia kote wanaweza kutumia alama na mandhari mbalimbali za kitamaduni kueleza falsafa ya msingi wa Zulu Nation.

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980, Zulu Nation ilianzisha matawi (yanayojitawala yenyewe) huko Japani, Ufaransa, Uingereza, Australia, Kanada, Korea Kusini na Cape Town nchini Afrika Kusini.

Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1980, katika kilele cha vuguvugu la Uafrocentriki katika hip-hop (wakati ambao wasanii kama vile KRS-One, Public Enemy, A Tribe Called Quest, Native Tongues, na Rakim walipata mafanikio), harakati hiyo ilionekana kujumuisha mafundisho mengi yanayohusiana na Nation of Islam, Nation of Gods and Earths , na Nuwaubian Nation. Katikati ya miaka ya 1990 baadhi ya wanachama walianza kuanzisha miradi au mashirika yao kama vile Ill Crew Universal.[3]

Afrika Bambaataa alijiuzulu kama kiongozi wa Zulu Nation mnamo Mei 2016 baada ya madai ya kuwanyanyasa kingono vijana na watoto kadhaa katika shirika hilo. Ronald Savage alikuwa wa kwanza kati ya wanaume kadhaa kumshutumu Bambaataa hadharani.

Mnamo mwaka wa 2017, mamia ya wanachama wa Zulu Nation walijiuzulu kutokana na kutokuwa na imani na kundi hilo na kuanzisha shirika lao la Zulu Union.

Zulu Nation nchini Ufaransa

[hariri | hariri chanzo]

Zulu Nation ilianzishwa Ufaransa mnamo 1982 na Afrika Bambaataa ziara ya "New York City Rap Tour" ilipotumbuiza nchini humo katika miji kadhaa (Paris, Lyon, Metz, Belfort, Mulhouse) na wasanii PHASE 2, Futura 2000, Dondi, Grandmaster D.ST, Rock Steady Crew, Rammellzee na kikundi cha Wasichana wawili wa Uholanzi, Buffalo Girls. Zulu Nation ilianzia katikati ya jiji la Par. Tangu mwaka wa 1987, uhusiano wa Zulu Nation na jumuiya ya muziki ya hip hop ya Ufaransa ulipungua. Baada ya ziara ya Afrika Bambaataa nchini Ufaransa mwaka wa 2008 na kuungana tena kwa Zulu Nation huko Paris, harakati mpya za Universal Zulu Nation zimeibuka katika miji tofauti nchini Ufaransa. [4] Kwa mujibu wa Veronique Henelon, "rap ya Kifaransa imekuwa ikionyesho uhusiano na Afrika."[5] Kipindi cha kwanza cha televisheni cha hip-hop kinaripotiwa kuonekana nchini Ufaransa. Kiliitwa 'H.I.P. H.O.P.' na kilionyeshwa na kituo cha TF1 mnamo 1984.

Wanachama mashuhuri na washirika

[hariri | hariri chanzo]

Katika tamaduni maarufu

[hariri | hariri chanzo]

Universal Zulu Nation imeangaziwa kwa urefu katika mfululizo wa filamu ya Netflix "The Get Down" iliyotoka mwaka 2016. Katika mfululizo huo, nafasi ya Afrika Bambaataa imeigizwa na mwigizaji mwenye asili ya Nigeria Okieriete Onaodowan.

  1. Chang, Jeff (2005). Can't Stop, Won't Stop: A History of the Hip-Hop Generation. New York: St. Martin's Press. ISBN 0-312-30143-X.
  2. About from ZuluNation.com, retrieved 28 September 2015
  3. "Wayback Machine". web.archive.org. 1997-04-09. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1997-04-09. Iliwekwa mnamo 2022-07-06.
  4. Prevos, A.J.M., "Post-colonial Popular Music in France: Rap Music and Hip-Hop Culture in the 1980s and 1990s." In Global Noise: Rap and Hip-Hop Outside the USA. Tony Mitchell ed., pp. 29–56. Middletown: Wesleyan University Press, 2001.
  5. Henelon, V. "Africa on Their Mind: Rap, Blackness, and Citizenship in France." In The Vinyl Ain't Final: Hip-Hop and the Globalisation of Black Popular Culture. Dipannita Basu and Sidney J. Lemelle, eds., pp. 151–66. London; Ann Arbor, MI: Pluto Press, 2006
  6. "Lil Wayne is Reportedly Joining the Hip-Hop Awareness Organization Zulu Nation". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-07-06. Iliwekwa mnamo 2022-07-06.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Universal Zulu Nation kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.