Nenda kwa yaliyomo

A Tribe Called Quest

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
A Tribe Called Quest

Maelezo ya awali
Asili yake Queens, New York, U.S.
Aina ya muziki Jazz rap, Alternative hip hop, Golden age hip hop
Miaka ya kazi 1985–1998
2006 -
Studio Jive Records
Ame/Wameshirikiana na Native Tongues Posse
De La Soul
Leaders of the New School
Black Sheep
Jungle Brothers
Busta Rhymes
Mobb Deep
Tovuti atribecalledquest.com
Wanachama wa zamani
Q-Tip
Phife Dawg
Ali Shaheed Muhammad
Jarobi White

A Tribe Called Quest ni kundi la muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani. Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1985, [1] na linaunganishwa na rapa/mtayarishaji Q-Tip, rapa Phife Dawg aka Phife Diggy (Malik Taylor), na DJ/mtayarishaji Ali Shaheed Muhammad.

Mwanachama wa nne, rapa Jarobi White, aliondoka kundini baada ya kutoa albamu yao ya kwanza na kurudi tena kundini mnamo mwaka wa 1991. Akiwa na De La Soul, kundi lilikuwa sehemu ya kati ya Native Tongues Posse, na wamefurahia mafanikio ya pamoja hasa baada ya kila kundi kuwa kimpango wake kwa mkusanyiko huo. Uvumbuzi wao unayeyusha hip hop na jazz umefanya uwe na mgongano mkubwa katika muziki wa hip hop, umesaidia kupanua wigo wa sanaa ya utayarishaji wa muziki wa hip hop.

Nyimbo zao nyingi kama vile "Bonita Applebum", "Can I Kick It?", "I Left My Wallet in El Segundo", "Scenario", "Check the Rhime", "Jazz (We've Got)", "Award Tour" na "Electric Relaxation" hutazamiwa kama classic na jumuiya za hip hop. Wametoa albamu tano kati ya 1990 na 1998. LP zao za kwanza zilikuwa maarufu mno, lakini kundi lilivunjika mnamo mwaka wa 1998. Mnamo 2006, kundi limeungana tena na kufanya ziara kadha wa kadha nchini Marekani, na kutoa ahadi ya kwamba watatoa albamu baada ya kufanya kazi katika mastudio kadha wa kadha.

Kundi hutazamiwa kama miongoni mwa makundi wavumbuzi wa alternative hip hop, kwa kusaidia kuweka njia ya kwa wasanii wapya wa hip hop.[2] John Bush wa Allmusic kawaita "kundi la rap lenye akili zaidi la miaka 1990,"[3] wakati wahariri wa About.com wamewapa nafasi ya #4 kwenye orodha yao "Makundi 25 ya Rap ya Muda Wote."[4]

Mwaka wa 2005, A Tribe Called Quest wamepata Tuzo ya Special Achievement Award kwenye Billboard R&B Hip-Hop Awards huko mjini Atlanta.[5] Mwaka wa 2007, kundi pia lilipewa heshima yake kwenye 4th VH1 Hip Hop Honors.

Discografia

[hariri | hariri chanzo]

Kompilesheni albamu

[hariri | hariri chanzo]
  1. "A Tribe Called Quest official site: Group biography". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-08. Iliwekwa mnamo 2012-05-29.
  2. "A Tribe Called Quest: Biography : Rolling Stone". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-16. Iliwekwa mnamo 2012-05-29. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  3. [A Tribe Called Quest katika Allmusic allmusic ((( A Tribe Called Quest > Biography )))]
  4. "25 Greatest Hip-Hop Groups - Best Rap Groups of All Time". Rap.about.com. 2012-01-26. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-05. Iliwekwa mnamo 2012-04-09.
  5. "Billboard Honors Khan, A Tribe Called Quest". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-29. Iliwekwa mnamo 2012-05-29.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:A Tribe Called Quest