Nenda kwa yaliyomo

Tulanana Bohela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tulanana Bohela
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwandishi wa habari

Tulanana Bohela ni mwanamke Mtanzania ambaye ni mwandishi wa habari, mtengeneza filamu na mpenda maendeleo ya jamii.

Amekuwa akifanya kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 7 hadi kufikia mwaka 2019 huku akiripoti mambo mbalimbali yanayojiri ukanda wa Afrika mashariki kwenye televisheni, redio na vyombo vingine vya kidijitali hasa kwa BBC Africa na BBC Swahili.[1]

Baadaye Bohela aliingia katika kitengo cha BBC World Service kama mwandishi na mzalishaji mkuu wa maudhui ya kidijitali.[2][3][4][5]

Kipaji na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Tulanana Bohela amekuwa maarufu kutokana na kazi mbalimbali anazozifanya ikiwa ni pamoja na uandishi wa habari na uzalishaji filamu,[6]mwanzilishi wa Snap Productions TZ[7] [8], mwanzilishi mwenza wa Ona stories[9], mzalishaji wa maudhui ya kidijitali na ripota wa habari za BBC[10][11], muongoza filamu[12] na mzalishaji wa maudhui ya kidijitali yajulikanayo kwa Kiingereza kama Virtual Reality (VR)[13] [14][15].

Kupitia kazi yake ya uandishi wa habari Bohela amekuwa mdau wa kutumia njia za kidijitali kuhamasisha usimulizi wa hadithi za Kiafrika na kukuza maendeleo ya Afrika hususani katika teknolojia, jamii na biashara.[16][17].Tulanana kwa wakati mwingine ni mzungumzaji katika mikutano mbalimbali hasa ihusuyo teknolojia[18] na mdau anayejishughulisha na kuzuia ndoa za utotoni kwa kuangazia matendo yahusuyo ndoa za utotoni barani Afrika[19][20]

Baadhi ya matukio muhimu nchini Tanzania ambayo Bohela amewahi kuripoti kama mwandishi wa habari wa BBC ni pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 nchini Tanzania,[21] kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar [22], kumwagiwa tindikali kwa wanawake wawili wa Uingereza huko Zanzibar[23] na kupinduka kwa kivuko cha MV Nyerere, moja ya matukio mabaya nchini Tanzania liliLOua watu wasiopungua 224 mwaka 2018.[24]

Kazi yake kwa kiasi kikubwa hujihusisha na utafiti wa utengenezwaji na ushirikishwanaji wa maudhui ya kidijitali barani Afrika.[25]

Mwaka 2017 Bohela alishinda shindano lijulikanalo kama #innovateAFRICA 2017 shindano lililolenga uvumbuzi na ubunifu wa namna video na simu vinaweza kutumika kutengeneza maudhui ya kidijitali. Pia akiwa mkerereketwa wa teknolojia iitwayo Virtual Reality (VR), Bohela alifanya onyesho la kwanza nchini Tanzania la VR wakati wa wiki ya ubunifu iliyofadhiliwa na HDIF na Kenyan VR production house, Black Rhino.[26]

Tuzo nyingine alizowahi kupokea ni pamoja na filamu yake ya Uthando iliyotangazwa na the Ousmane Sembene Award at the Zanzibar International Film Festival huku pia akishinda kama Muongoza filamu bora akiwa huko Afrika Kusini.[27][28][29].

  1. http://www.sheroes.co.tz/sheroes.html Archived 8 Machi 2019 at the Wayback Machine. iliangaliwa tar 7 March 2019
  2. "Zanzibar votes in re-run election". BBC News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-06-20.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-07. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  4. https://ela-newsportal.com/bbc-african-service-covers-elearning-africa/
  5. https://www.ted.com/tedx/events/13353
  6. https://www.dfa.ie/irish-embassy/tanzania/news-and-events/2016/women-in-liberation-event/
  7. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  8. https://www.ted.com/tedx/events/13353
  9. https://arvrjourney.com/meet-the-3rd-annual-electric-south-ar-vr-lab-creators-e2afd30056e9
  10. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-07. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  11. https://www.bbc.com/news/av/world-africa-35855804/zanzibar-votes-in-re-run-tanzanian-election
  12. http://film.britishcouncil.org/calendar/2018/were-off-to-sheffield-docfest
  13. https://futureoffilm.virtualconference.com/
  14. http://film.britishcouncil.org/calendar/2018/were-off-to-sheffield-docfest
  15. https://www.svaff.org/index.php?option=com_content&view=article&id=72:everyones-child-85-mins&catid=11:feature-films&Itemid=6
  16. https://www.slideshare.net/TulananaBohela
  17. https://www.youtube.com/watch?v=lGGepGPu3oY
  18. https://www.youtube.com/watch?v=lGGepGPu3oY
  19. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-09. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  20. https://www.svaff.org/index.php?option=com_content&view=article&id=72:everyones-child-85-mins&catid=11:feature-films&Itemid=6
  21. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-09. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  22. https://clubofmozambique.com/news/voters-in-benin-cape-verde-congo-niger-senegal-and-zanzibar-go-to-polls/
  23. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-08. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  24. https://www.trtworld.com/africa/survivor-pulled-from-capsized-tanzanian-ferry-as-death-toll-reaches-224-20392
  25. https://www.youtube.com/watch?v=lGGepGPu3oY
  26. https://arvrjourney.com/meet-the-3rd-annual-electric-south-ar-vr-lab-creators-e2afd30056e9
  27. https://www.ted.com/tedx/events/13353 iliangaliwa 7March 2019
  28. https://www.flickr.com/photos/61526027@N05/19982255336
  29. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-07. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tulanana Bohela kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.