Nenda kwa yaliyomo

Theodori na Theofane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu wa Mt. Theodori.
Picha takatifu ya Mt. Theofane.

Theodori na Theofane (Yerusalemu, leo nchini Israeli/Palestina, 775/778 hivi - Hisarlik, Bitinia, leo nchini Uturuki, 842 hivi / Nisea, leo nchini Uturuki, 845) walikuwa ndugu wamonaki, waliodhulumiwa na serikali ya Dola la Roma Mashariki kwa sababu ya kutetea heshima kwa picha takatifu.

Hatimaye Theodori alifariki gerezani kutokana na majeraha aliyotiwa, kumbe mdogo wake akawa askofu mkuu wa Nisea kuanzia mwaka 842 hadi kifo chake. Pia alipata umaarufu kwa kutunga tenzi nyingi.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 27 Desemba[1], lakini katika Ukristo wa Mashariki Theofane anaheshimiwa peke yake tarehe 11 Oktoba.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.