Sudi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Sudi ni kata ya Wilaya ya Lindi Vijijini katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,544 [1] walioishi humo.

Msimbo wa posta ni 65202.

Eneo na historia[hariri | hariri chanzo]

Sudi iko kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi kati ya Lindi na Mikindani, sehemu ambapo Mto Mambi unaishia.

Kabla ya ukoloni na wakati wa utawala wa Kijerumani ilikuwa moja ya bandari za maana kwenye mwambao wa kusini mwa Tanzania ya leo. Mnamo mwaka 1900 ilikuwa na wakazi 2,000. Mnamo mwaka 1900 mfanyabiashara mkuu alikuwa mmoja Mohamed Chamdu[2].

Ilisemekana iliundwa na Mwarabu tajiri aliyefanya biashara huko. Wajerumani waliunda hapa ofisi ya forodha. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Sudi ilikuwa kituo muhimu cha kijeshi cha Wajerumani; meli zilizoleta ramia na mahitaji ya kijeshi ziliweza kujificha katika hori ya Sudi inayofanywa na mdomo mpana wa Mto Mambi. Kwenye Septemba 1916 Sudi ilivamiwa na Waingereza[3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf Sensa ya 2012, Lindi - Lindi DC]
  2. Kolonialhandbuch 1903, uk. 253
  3. Lochner, uk. 356

Vitabu[hariri | hariri chanzo]

  • Rudolf Fitzner: Deutsches Kolonial-Handbuch, Band 1, toleo la 8, Berlin 1908, *Rochus Schmidt: Deutschlands Kolonien. Band 1, Berlin: Verlag des Vereins der Bücherfreunde Schall & Grund, 1898 (Reprint na Weltbild Verlag, Augsburg 1998, ISBN 3-8289-0301-0)
  • Reinhard K. Lochner: Kampf im Rufiji-Delta. München, 1987, S. 356, ISBN 3-453-02420-6
  • Makala "Ssudi", katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (Deutsches Kolonial-Lexikon / ed. Heinrich Schnee. - Leipzig : Quelle & Meyer 1920. - Vitabu 3,) online hapa
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Lindi Vijijini - Mkoa wa Lindi - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chiponda | Kilangala | Kilolambwani | Kinyope | Kitomanga | Kiwalala | Kiwawa | Longa | Majengo | Mandwanga | Matimba | Mchinga | Milola | Mipingo | Mnara | Mnolela | Mtama | Mtua | Mtumbya | Mvuleni | Nachunyu | Nahukahuka | Namangwale | Namupa | Nangaru | Navanga | Nyangamara | Nyangao | Nyengedi | Pangatena | Rutamba | Sudi


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sudi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.