Steve Tikolo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Stephen Ogonji Tikolo (amezaliwa 25 Juni 1971 mjini Nairobi) ni mchezaji kiriketi kutoka nchini Kenya.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Yeye ni “middle order batsman’ anayetumia mkono wa kulia na wakati mwingine wa ” medium pace bowler” wa mkono wa kulia. Yeye hutupa mpira huo wa kriketi kwa ufanisi kabisa katika fomu fupi ya mchezo huo. Tikolo awali ameiwakilishwa Border ambayo ni klabu ya kritketi nchini Afrika Kusini na pia ametumia muda akicheza kriketi katika nchi za Uingereza na Bangladesh. Hivi majuzi amekuwa akicheza Kriketi ya klabu katika sehemu ya Haverigg na akirudi nyumbani yeye huichezea klabu ya Kriketi ya Swamibapa katika mji mkuu wa Nairobi. Aliwahi kuicheza timu ya kriketi ya wachezji 11 kutoka nchi tofauti za Afrika mara moja dhidi ya Asia.

Amekuwa mfungaji bora na maarufu na anahesabiwa kuwa mmoja wa wachezaji bora wanaojulikana kutoka nchi Kenya. Anaonekana kama mchezaji mkuu katika nchi yake ya nyumbani na hata anaonekana kwa wengi kama mchezaji bora kutoka nchi shirika, ingawa sasa amepata ushindani kutoka kwa Ryan ten Doeschate. Tikolo amehodhi kama kwamba mnamo Januari 2007 alikuwa na alama sita za juu zaidi kuweza kufungwa na “batsman” kutoka Kenya katika Kriketi ya ODI. Tikolo ameunda karne tatu za ODI; 106 * dhidi ya Bangladesh, 111 dhidi ya Bermuda na 102 dhidi ya Zimbabwe. Ameondolewa katika za alama za 90 katika hafla ya tatu.

Tikolo alitoka katika familia ya kriketi kwani kakake mkongwe Tom alikuwa nahodha wa zamani wa Kenya huku kakake mwengine David Tikolo alicheza katika Kombe la Dunia la mwaka wa 1996. Ilikuwa katika mchuano huu ambapo Steve alicheza mechi yake ya kwanza ya ODI kwa Kenya. Akija katika wakati wa 3 katika miingio yake ya kwanza alitengeneza 65 dhidi ya Wahindi hao. Aliendelea kucheza miingio mingine ya kuvutia zaidi katika Kombe hilo, akawa mfumgaji bora wa upande wake na mikimbio 29 katika ushindi wao wa kihistoria dhidi ya West Indies katika Pune na kutengeneza 96 dhidi ya Sri Lanka katika Kandy.

Tikolo aliendeleza zaidi sifa yake kama “batsman” bora zaidi wa Kenya akiwa na 147 dhidi Bangladesh katika fainali ya nyara ya ICC mwaka wa 1997. Miingio hii iliwapa Kenya rasmi hali ya ODI na kuwapa Kenya nafasi kushiriki katika kombe la dunia la mwaka wa 1999 ambalo mwenyeji wake alikuwa Uingereza. Hili lilikuwa kombe lingine la dunia lenye mafanikio kwa Steve Tikolo kwani alitengeneza jozi za 50 dhidi ya India na Uingereza.

Mwaka wa 2002 alitajwa kama nahodha mpya wa Kenya na aliongoza kutoka mbele katika nyara ya Mabingwa na miingio ya 93 na 69.

Tikolo aliongoza timu ya kitaifa ya Kenya wakati walishiriki katika nusu fainali ya kombe la dunia la kriketi mwaka wa 2003. Hii ilikuwa mafanikio makubwa kwa nchi ya Kenya ambayo bado haijapewa hali za Test.

Baada ya maonyesho mabaya katika nyara ya Mabingwa mwaka wa 2004, alijiondoa kama nahodha na badala yake aliongoza mgomo wa wachezaji katika maandamano ya siasa za ndani. Mgomo huu ulilazimisha serikali mpya ndiposa akarejea kama nahodha.

Mwaka wa 2005 Tikolo alisainiwa na klabu ya Haverigg iliacheze Kriketi nchini Uingereza.

Mwaka wa 2007 akawa mchezaji wa kwanza kutoka nchi isiyo cheza jaribio (non test playing country) kushiriki katika michezo 100 ya ODI. Mwaka wa 2008 Steve Tikolo alitajwa kama nahodha wa Eastern Aces katika mchuano wa nchi ya Kenya, Sahara Elite League.

Tikolo atastaafu baada ya msimu wa 2009. Mchuano mkuu wake wa mwisho, na mechi yake ya mwisho kama nahodha, ilikuwa katika mechi ya kufuzu kushiriki katika kombe la dunia la ICC mwaka wa 2009, ambapo Kenya ilifuzu kushiriki katika kombe la dunia la Kriketi la mwaka wa 2011.

Wakati Tikolo hachezi kriketi yeye hucheza mchezo wa ndani wa “indoor bowls”.

Karne za ODI[hariri | hariri chanzo]

ODI centuries of Steve Tikolo
Mikimbio Mechi Mpinzani Mji Mkuu/Nchi Ukumbi Mwaka
[1] 106* 21 Bangladesh Dhaka, Bangladesh Bangabandhu National Stadium 1999
[2] 111 82 Bermuda Mombasa, Kenya Mombasa Sports Ground 2006
[3] 102 107 Zimbabwe Nairobi, Kenya Gymkana Club Ground 2008

Karne za Daraja la Kwanza[hariri | hariri chanzo]

First class centuries of Steve Tikolo
Mikimbio Mechi Wapinzani Mji Mkuu/Nchi Ukumbi Mwaka
[1] 110 12 Zimbabwe A Nairobi, Kenya Gymkhana Club Ground 2001
[2] 115* 13 Zimbabwe A Nairobi, Kenya Simba Union Ground 2001
[3] 117 15 Sri Lanka A Matara, Sri Lanka Uyanwatte Stadium 2002
[4] 109 26 Pakistan A Nairobi, Kenya Simba Union Ground 2004
[5] 156 29 India A Nairobi, Kenya Simba Union Ground 2004
[6] 149 30 Uganda Kampala, Uganda Lugogo Stadium 2005
[7] 220 34 Bermuda Windhoek, Namibia United Ground 2005
[8] 177* 35 Ireland Windhoek, Namibia Wanderers Cricket Ground 2005
[9] 212* 36 Netherlands Nairobi, Kenya Gymkhana Club Ground 2006
[10] 158 47 Canada Toronto, Canada Maple Leaf South-West Ground 2009
[11] 169

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Notable Joluo