Sinki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sinki la bafuni.

Sinki (kutoka Kiingereza: sink; inajulikana pia kwa majina mengine ikiwa ni pamoja na bakuli la kunawia, beseni la mkono) ni bakuli linalotumika kusafisha mikono, vifaa vya kupikia na kula na madhumuni mengine. Sinki huwa na bomba linalotoa maji baridi na moto na shimo la kupitisha maji machafu. Wakati mwingine sinki hujengwa na kifaa cha kutoa sabuni. Mara nyingi sinki, hasa jikoni hujengwa karibu au ndani ya kaunta.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mchoro wa mwanamke akisafisha mikono kwenye sinki.

Sinki la bafuni lilianza nchini Marekani mwishoni mwa karne ya 18. [1] Sinki hili lilijumuisha meza ndogo, bakuli na beseni kufuatia mila ya Uingereza. Wakati mwingine meza ilikuwa na shimo ambapo bakuli kubwa liliwekwa, ambalo lilisababisha kutengenezwa kwa sinki kavu. Kutoka mwaka wa 1820 hadi 1900, sinki kavu lilijumuisha kabati ya mbao pamoja na madini ya zinki au risasi ambapo bakuli ya maji ilihifadhiwa.

Sinki la jikoni linaaminika kuwa lilianza kutumika kama miaka 200 iliyopita[2]. Umbo na utengenezwaji wake umebadilika sana toka ilipoanza kutumika hadi hivi sasa [3].

Vifaa[hariri | hariri chanzo]

Sinki hutengenezwa kwa kutumia vifaa mbalimbali kama vileː {div col|colwidth=20em}}

Picha[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina mbalimbali za sinki kama inavyoonekana kwenye picha hiziː

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sinks. The Old-House Journal; August 1986, Vol. 14, No. 6: page 270 - 277. Published by Active Interest Media, Inc. ISSN 0094-0178
  2. Kitchen Sinks Have a History
  3. Kitchen sinks

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]